AMKA NA BWANA LEO 12
*KESHA LA ASUBUHI.*
Jumatatu, 12/04/2021.
*WEMA, SIFA YA KIMAADILI.*
*Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana. Efeso 6:4.*
▶️Mungu anatoa wito kwa kila muumini kukoma kutafuta makosa, kuacha kuropoka na kutoa maneno makali. Wazazi, hebu maneno mnayoyatamka kwa watoto wenu yawe mema na mazuri ili kwamba malaika wapate msaada wenu katika kuwavuta kwa Kristo. Matengenezo kamili yanahitajika kufanyika katika makanisa yetu ya nyumbani. Hebu yaanze upesi. Manung’uniko, maudhi, makaripio yote yakome. Wale wanaoudhi na kukaripia wanawafungia nje malaika wa mbinguni na kuwafungulia mlango malaika waovu.
▶️Hebu mume na mke wakumbuke kuwa wanao mzigo wa kubeba pasipo kuyafanya maisha yao kuwa dhalili kwa kuruhusu utofauti kuingia kati yao. Wale wanaotoa nafasi ya tofauti ndogondogo wanamkaribisha Shetani katika nyumba yao. Watoto wanachukua roho ya ugomvi juu ya jambo dogo. Mawakala waovu wanafanya sehemu yao kuwafanya wazazi na watoto kutokuwa watii kwa Mungu.
▶️Ndugu na dada zangu, je! hamtakuwa watendakazi pamoja na Mungu mkifanya kazi kwa amani na upatano. Omba kwa ajili ya mvuto mzuri wa Roho Mtakatifu. Acha midomo yako itawaliwe na sheria ya wema. Kataa kuwa mkali, asiye na heshima, na wema. ishi kulingana na madai ya imani yako...
▶️Unapokubali kuvaa nira ya Kristo na kutii wito “ Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;” (Mathayo 11:29), utaacha kuweka nira katika shingo za wengine. Utaacha kuwatafuta makosa. Hutaendelea kuchukulia kama ni sifa ya kimaadili kutofautiana na wengine. Utasimama katika hoja zile unazoweza kuzikubali.
▶️Tunajiandaa kukutana na Bwana wetu ajapo katika mawingu ya mbinguni akiwa na nguvu na utukufu mwingi. Katika kazi hii kuu na ya wema tunatakiwa kusaidiana. Wazazi wanatakiwa kuleta furaha na kila uzuri wawezao katika nyumba zao. Wanatakiwa kuifanya nyumba yao kuwa ya furaha tele kwa maneno na matendo mema
Post a Comment