mpende Mkeo na sio Familia ya zamani
BY MWALIMU HABELNOAH
JM LIBRARY
MWANZA
UJUMBE HUU UMENILIZA BILA KUJUA KUWA NALIA NINI!!
Babu mmoja aling’ng’ania kwenda mjini kwenye harusi ya mjukuu wake, pamoja na hali yake ya kiafya kuwa mbaya lakini alitaka hivyo. Alihudhuria na siku ya harusi baada ya sherehe alimuomba mjukuu wake aongee naye kabla hawajaenda honeymoon.
Watu walitaka asubiri kwanza lakini aliwaambia hapana, mjukuu aliitwa na alianza kuongea naye. “Mjukuu wangu najua sina muda sana ila kuna kitu nataka kukuambia, leo umeoa sitaki ufanye kosa kama nililofanya mimi na alilofanya Baba yako. Baba yako nilimfundisha kua wanawake si watu wa kuaminiwa na unapaswa kuamini familia kwanza.
Nilikosea na ndiyo maana leo pamoja na kuwa Bibi yako bado yupo lakini nakufa mpweke. Ukweli nikua mjukuu wangu mkeo ndiyo anapaswa kuwa namba moja kwako kwa kila kitu kwani huyo ndiyo mtu pekee ambaye utazeeka naye na utakufa pembeni yake.
Mimi nilimpenda Mama yangu kuliko Bibi yako, lakini leo hayupo, nikawapenda Dada zangu lakini leo wanakufa na waume zao, nikawapenda Kaka zangu lakini leo wanakufa na wake zao. Mtu pekee ambaye nilimdharau na kumnyanyasa ni Bibi yako na ndiye ambaye tumetelekezwa naye Kijijini.
Angalia Baba yako, walikua wakipendana sana na Baba zako wadogo lakini leo wako wapi, kila mmoja anakufa na wake. Hivyo mjukuu wangu kama ukimpenda mkeo sasa basi wakati mkiwa wazee hutakua ukijuta hasa ukikumbuka kuwa ulimtesa zamani kama mimi ninavyojuta sasa.
Mjukuu wangu mtu hazeeki na Mama yake, mwanaume ambaye huzeeka akiwa anaishi kwa Mama yake huyo si mwanaume ni Dung’uthi, mwanaume ambaye huzeekea akiwa anaishi kwa Dada yake huyo ni Zezeta na mwanaume ambaye huzeeka akiwa anaishi kwa Kaka yake huyo ni Kapuku ila ambaye huzeeka na mkewe huyo ndiyo Mwanaume.”
Babu alimaliza kuongea na kuwaruhusu wajukuu zake kwenda kusherehekea harusi yao. Siku tatu baadaye babu alifariki akiwa pembeni ya mkewe “Bibi”, mwanamke ambaye alitumia ujana wake wote kumnyanyasa. Maneno ya Babu yalitimia, alikufa pemeni ya mwanamke aliyekua akimnyanyasa na kumuona kama takataka.
Kuna #SHARE ngapi kwa Babu?
Imetungwa na mwalimu habelnoah
Post a Comment