mafunzo ya watu wazima leo 25

LESONI, MACHI 25

SOMO: “NDIVYO UZAO WENU NA JINA LENU LITAKAVYOKAA” (ISA. 66:22—24)



Soma Isaya 66:22. Aya hiyo hutuambia nini? Ni tumaini gani tunalopata hapo?



Moja ya ahadi kuu za pekee katika Isaya inapatikana katika Isaya 66:22. Isome kwa makini. Katika mbingu mpya na nchi mpya, uzao wetu na jina letu litadumu milele. Hakuna kufutwa, kukatwa, kuondolewa, kupogolewa, au kung’olewa. Tunayo hapa ahadi ya uzima wa milele katika ulimwengu uliofanywa upya—usiokuwa na dhambi, usiokuwa na mauti, usiokuwa na mateso, mbingu mpya na nchi mpya, utimilifu na ukamilifu wa mwisho wa imani yetu ya kikristo, kilele cha kile Kristo alichokamilisha kwa ajili yetu pale msalabani. 



Kwa nini ipo kauli ya mwezi mpya katika sabato zisimuliwazo katika mbingu mpya na nchi mpya kama ielezewavyo katika Isaya 66:23? 



Japo kuna njia tofauti za kushughulikia aya hii ngumu, mtazamo mmojawapo ni huu: Mungu aliumba Sabato mapema kabla kaida za kafara hazijaanza (Mwanzo 2:2, 3). Hivyo japo Sabato iliheshimika katika kaida za kafara, haikuzitegemea. Hivyo, Sabato zinaendelea pasipo kutibuliwa katika zama zote za urejeshwaji, hadi kuingia nchi mpya. Hakuna ishara yo yote katika Biblia kuwa miezi mipya ilikuwa siku halali za ibada nje ya mfumo wa kaida za kafara. Ila yumkini zitakuwa siku za ibada katika nchi mpya (japo siyo kwa hadhi kuu kama ilivyo Sabato ya kila juma), yumkini kulingana na ratiba ya kila mwezi ya mti wa uzima (Ufunuo 22:2). Japo maana halisi ya Isaya 66:23 haipo dhahiri, jambo kubwa la msingi tulipatalo hapo ni kwamba watu wa Mungu watakuwa wakimwabudu Mungu kwa umilele wote. 



Kwa nini Isaya huishia na picha dhalili ya waliookoka wakitazama mizoga ya waasi walioangamizwa na Mungu (Isa. 66:24)?



Isaya alitoa onyo kwa watu wa zama zake, akilinganisha kile kitakachowasibu waaminifu waliookoka toka uangamivu wa Babeli dhidi ya waasi ambao wataangamizwa. Hii haiongelei moto au mateso ya umilele—hapa waovu wamekufa, wameuawa kwa “moto”, uangamivu ambao haukuzuiwa hadi pale ulipoikamilisha kazi yake ili kwamba uumbaji upya wa Yerusalemu uanze. 



Usia wa onyo wa Isaya huelekeza kwenye utimilifu uliotabiriwa katika kitabu cha Ufunuo: kuangamizwa kwa wenye dhambi, Shetani, na mauti katika ziwa la moto (Ufunuo 20), ambapo baada ya hapo zitakuwepo “mbingu mpya na nchi mpya,” na Mji mtakatifu wa “Yerusalemu Mpya”, wala hakutakuwepo maombolezo wala maumivu tena, “kwani mambo ya kwanza yamekwisha kupita” (Ufunuo 21:1—4; linganisha na Isa. 65:17—19), maisha mapya, ya uzima wa milele kwa wote waliokombolewa kutoka duniani. 

No comments