AMKA NA BWANA LEO 31

KESHA LA ASUBUHI

JUMATANO, MACHI, 31, 2021
SOMO: MILKI YAKE ALIYOINUNUA 

Maana silaha ya vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome. Tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu, na tukiteka nyara kila fikra ipate kumtii Kristo. 

2 Wakorintho 10:4, 5. 



Katika kushughulika na watu wasio na busara na waovu, wale wanaoiamini kweli wanapaswa kuwa waangalifu wasijishushe wenyewe katika kiwango sawa nao, ambapo watatumia silaha zile zile za kishetani ambazo adui zao hutumia, kwa kuachia huru mawazo binafsi yenye nguvu, wakiinuka dhidi yao wenyewe na dhidi ya kazi ambayo Bwana amewapatia waifanye, uchu na uadui mkali. 



Endeleeni kumwinua Yesu. Tu watenda kazi pamoja na Mungu. Tumepatiwa silaha za kiroho, zenye nguvu katika kuangusha ngome za adui. Ni lazima katika jambo tusiiwakilishe imani yetu kwa kuchanganya sifa zisizo kama za Kristo katika kazi yake. Ni lazima tuinue sheria ya Mungu, kama inayotufungamanisha na Kristo na wote wanaompenda na kuzishika amri zake. Pia tunapaswa kuudhihirisha upendo kwa roho ambazo Kristo amezifia. Imani yetu inapaswa kudhihirishwa kama nguvu ambayo Kristo ndiye mwenye kuianzisha. Na Biblia, Neno lake, linapaswa kutufanya wenye hekima ili kuufikia wokovu. 



Hebu haki ya Kristo, na mvuto wake unaotoa uzima, katika nafsi, na kisha unaweza kuimba, Amesamehe dhambi zetu zote. Unasema, nimejawa ugonjwa wa kiroho. Tabibu mkuu anakuita uje kwake, ili aweze kukuponya. Anaponya magonjwa yetu yote. Ugonjwa mbaya kabisa kuliko magonjwa haya ni husuda, wivu, shuku mbaya, matukano, tamaa ya kufuata mipango ambayo huleta upinzani kwa kazi ya Mungu. 



Maisha ya wote wanaopaswa kuwa watakatifu, lakini yamejawa upotovu, na kwa sababu hii, wanadamu kwa urahisi wanatumikishwa chini ya majaribu ya Shetani. Bali ikiwa Kristo anakaa ndani ya moyo wako, waweza kusema, Yeye huokoa maisha yetu kutoka katika uharibifu: Yeye hutuvika kwa wema na rehema ya upole. Kisha ruhusu nyimbo za sifa ziwe katika midomo yetu na katika mioyo yetu. 



Tafakari juu ya mateso ya Yesu kwa ajili yetu. Badala ya kutazama na kupata kitu cha kushitaki na kulaumu kwa wengine, mshukuru Bwana kwake kuna msamaha. Kristo huhuzunishwa tunapokosoa na kushutumu; kwa maana hii ni kazi ya Shetani. Hebu tuchote maji toka katika visima vya wokovu, na kumsifu Bwana. 



Si kuhubiri kunakotoa uthibitisho kwamba nafsi imezaliwa upya. Kuutambua upole wa Kristo kuwaelekea kondoo wa malisho yake hutoa uthibitisho wa hili. 

No comments