AMKA NA BWANA LEO 1
KESHA LA ASUBUHI
Alhamis 01/04/2021
*KUKIDHI VIGEZO*
*Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.* *Wakolosai 4: 5, 6*
Hebu shughuli zisikuzwe kiasi kwamba muda unatumika kwa mahangaiko yasiyokuwa muhimu. Uzito wa suala hili umekuwa ukihimizwa sana akilini mwangu kwa mkazo nisioweza kuueleza. Wakati unapita, na ninapooneshwa makanisa mengi ambayo hayajaandaliwa kufanya kazi kwa ajili ya Bwana, bali yapo katika hali ya kutokujali, ninatahadharishwa na kujiuliza, niseme nini au nifanye nini ili kubadili mpangilio uliopo wa mambo? Ninaweza kusema, *" itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote, akipata hasara ya nafsi yake? Ama mtu atoe nini badala ya nafsi yake? ( Marko 8:36, 37)*
Ninafikiri hakuna hata mmoja kati yetu aliye katika hali ya kutambua kuwa ni lazima tuwe watendakazi pamoja na Mungu. Wengi hawaelewi maana ya uongofu halisi unachohusisha. Na sasa ninakujulisha wewe na familia yako kwamba waweza kupata mwamko na kuguswa na jukumu la dhati la kutaka kuwaamsha watambue hitaji la kukesha na kutafuta kuziokoa roho zinazopotea bila Kristo. *Kila siku muonye mtu fulani ambaye bado hajui kuwa mwisho wa mambo yote upo karibu.*
Hakuna yodi wala nukta moja ya vigezo vitakatifu vya Mungu itakayobadilishwa kumfaa mwanadamu katika hali yake ya kutokuwa tayari. Neno lake takatifu halitabadilika wala kukoma. Ulimwengu umesinzia katika dhambi zao. Mbingu na nchi zitapita lakini Neno lake halitapita kamwe. *Sisi sote twapaswa kuongozwa na Neno la Mungu. Ni kazi iliyoje iliyoko mbele yetu na wanaodai kuwa Wakristo bado hawatambui! *"Msipoongoka na kuwa kama vitoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.” (Mathayo 18:3.)*
*Ni wachache kama nini wanaotambua mvuto wa mambo madogo katika maisha haya. Wale watakaostahimili kujaribiwa, upimaji wa Mungu, Kristo atawakiri. Ukweli, ukweli uokoao wa Neno la Mungu, tukiuishi, utatufanya tufae kuwa sehemu ya jumuia ya waliokombolewa. Mungu tusaidie kuthamini ubora wa maadili. Ubora wa mawazo safi yaliyotakaswa ni ya thamani sana kuliko dhahabu ya Ofiri. Utengenezaji wa msimamo wa kweli wa kimaadili pamoja na Mungu ni kazi ya maisha yote. Fundisha haya, kaka na dada zangu kwa maadili na kwa vielelezo.*
*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI MPENDWA*
Post a Comment