PROF. LIPUMBA; JPM TEKELEZA KATIBA MPYA

Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ametoa wito kwa Rais John Magufuli kutekeleza mchakato wa Katiba Mpya inayotokana na mapendekezo ya Wananchi wa Tanzania.

Kwenye hotuba yako ulipokuwa unazindua bunge Novemba, uliwaeleza wabunge kuwa katika kipindi chako cha mwisho utahakikisha yale uliyoyaahidi unayatekeleza, na moja ya ahadi zako ni kiporo cha Katiba mpya ambacho Watanzania wengi walishiriki kutoa maoni yao, nakukumbusha kulifanyia kazi suala hilo." Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti CUF Taifa akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Sheria na miaka 100 ya Mahakama, Dodoma.
#BinagoUPDATES

No comments