mafunzo ya watu wazima leo 24

LESONI, FEBRUARI 24

SOMO: TUMAINI KABLA YA WAKATI KUFIKA 



Ukweli kwamba Isaya alimtabiri kwa usahihi Koreshi kwa jina huwasumbua watu wasioamini kwamba manabii hupokea utabiri kutoka kwa Mungu. Ili kukabiliana na hilo, wanakubali nadharia kwamba nabii mwingine, “Isaya wa pili,” aliyeishi wakati wa Koreshi, aliandika Isaya 40—66. Hivyo, kitabu cha Isaya “kimekatwa mara mbili,” janga kama hilo hueleweka kimapokeo kumfika nabii mwenyewe (tazama Eb. 11:37). 



Hakuna, hata hivyo, ushahidi wa kihistoria wa kuwepo kwa “Isaya” wa pili. Ikiwa alikuwepo, ingekuwa ajabu Biblia kutomtaja, kwa kuwa ujumbe wake ni wa muhimu sana, na ustadi wa uandishi wake ni wa ajabu sana. Hata katika maandiko ya kale kabisa ya Biblia, gombo la Isaya kutoka magunduzi ya kiakiolojia ya Qumran, havina mgawanyiko kati ya Isaya 39 na 40 ambao ungeonesha mpito kwenda kwa mwandishi mpya. 



Ujumbe wa msingi wa Isaya haubadiliki katika kitabu chote: Mtumainini Mungu wa kweli, pamoja na Mkombozi wake wa kimasihi, kuliko mamlaka zingine. Wanazuoni husisitiza kuhama kwa mkazo wa fikra kutoka katika kipindi cha Ashuru katika Isaya 1—39 kwenda kwa kipindi cha Babeli katika sura ya 40 zinazofuata. Lakini tumegundua kwamba Isaya 13—14 na 39 zilishatoa wazo la utumwa wa Babeli. Ni kweli kwamba Isaya 1—39 husisitiza juu ya hukumu na Isaya 40—46 husisitizia faraja. Lakini katika sura za awali faraja ya Kiungu na matumaini ni tele pia, na vifungu vinavyofuata, kama vile Isaya 42:18—25, Isaya 43:22—28 na Isaya 48:1—11, huzungumzia hukumu ya Mungu kwa Yuda kwa kumwacha. Kwa hakika, utabiri wa Isaya wa faraja ya wakati ujao humaanisha kwa wakati uo huo. 



Japo taifa halikukabiliwa na janga la kutisha kwa sababu ya dhambi za watu, wengine miongoni mwao hawakukata tamaa. Walishikilia ahadi za Mungu, kama vile katika Mambo ya Walawi 26:40—45. Soma mafungu hayo kwa makini. Jiweke katika nafasi ya hao Waebrania waliokuwa hai baada ya kushindwa na Babeli. Ni tumaini gani ungepata katika maneno haya? 



Ni kanuni gani za kiroho unaona zikitenda kazi katika mafungu hayo ya Mambo ya Walawi? Mungu anasema nini kwa Israeli hapo? Kanuni hizo hutendaje kazi katika maisha yetu wenyewe? 

No comments