KAULI KONKI ZA ZLATAN ✍

MDAU:-BAADHI YA KAULI KONKI ALIZOWAHI KUZIONGEA ZLATAN IBRAHMOVIC.

"Simba huwa hawafananishwi na binadamu...wanajifananisha wao kwa wao"

Akimaanisha yeye Simba usimfananishe na Wachezaji (binadamu) wenigine...Dah.

"Siufuatilii Mpira ila Mpira ndio unanifuatilia Mimi".

"Kama ningeambiwa nichague mmoja wapo Kati ya Lingard (Jesse) AU Jones(Phil)...Basi nitachagua AU".

Akimaanisha hawezi kumchagua hata mmoja wao.

"Kwenye safari yangu ya kucheza Mpira...Sihitaji Kocha ili nifanikiwe...Makocha ndio wananihitaji mimi ili wafanikiwe".

Mwandishi :
 Unajisikiaje baada ya kufunga goli?

Zlatan:
Liulize goli linajisikiaje baada ya kufungwa na Mimi?

"Huwa siu-controll Mpira...ila Mpira unaji-control wenyewe kwaajili yangu".

"Nikiwa najiangalia kwenye kioo huwa siioni taswira yangu kwakuwa hakujawahi kuwa na Zlatan (Ibrahimovic) wawili".

 Mwandishi:
Unajichukulia mwenyewe kuwa wewe ni SIMBA na kuwataja Ronaldo na Messi kama binadamu Lakini wao wana Balloon d'Or ambazo wewe hauna.

Zlatan:Huwa sijali Kuhusu Tuzo Binafsi...Ningekuwa nazihitaji Basi ningeenda kucheza golf.

"Natumia Miguu yangu miwili kucheza Mpira Lakini Natumia mwili wangu wote kufunga magoli".

"Ninapochelewa mazoezini...Wachezaji wenzangu ndio huwa wanaadhibiwa kwa kuwahi kabla yangu".

"Ukinikaribisha nyumbani Kwako...Wewe ndiye Utakuwa mgeni wangu".

Huyo ndio Zlatan bhana 😂
#BinagoUPDATES

No comments