JPM; TUMUAMINI MUNGU TUU, NA TUENDELEE KUJIFUKIZA TANZANIA HAKUNA CORONA

“Hakuna kitakachoshindikana, Mungu ni Mshindi, Tanzania tumeshinda, tuendelee kuchukua tahadhari, kuna dawa nyingi nzuri za kujifukiza, kuna Covidol,Bupiji zile zinafanya kazi, zimethibitishwa na Mkemia Mkuu na zinaleta reaction ya ku-affect kwenye virus na bacteria by 99.9%”-JPM 

"Leo mmenifurahisha sana, Jeshi la Magereza nililokuwa nimelizoea kila siku unakuta mambo ya kukuudhi leo mmenifurahisha, lakini pia leo nilitembelea Gereza la Isanga, nimeona sehemu ya Watu walipokuwa wananyongwa, panatisha, panatisha”-JPM

“Watumieni vizuri hawa Wafungwa, ndio mbinu za Nchi zilizoendelea zinawatumia Wafungwa kuzalisha mali, pia nimeweka jiwe la msingi la kiwanda cha samani hapa Msalato ambacho kitagharimu Bil 2 (fedha za Serikali), ambapo hadi Mil 820.3 zimetolewa, Bil 1.18 tutaimalizia”-JPM 

“Mmeniambia juu ya Wastaafu 331 wanaodai jumla ya Tsh. Milioni 546.1 kwa ajili ya nauli na mizigo yao, Waziri wa Mambo ya Ndani fuatilia Wizara ya Fedha na Mipango ili Wastaafu hawa wote walipwe malipo yao mapema, hakuna sababu ya Mtu amestaafu halafu anaanza kuhangaika”-JPM 

“Hata hilo la uniform mkiamua mtaweza, kweli katika Wafungwa hao wote hakuna anayejua kushona nguo kwa cherehani, ina maana Nchi hii mafundi cherehani hawafungwi?, kama wapo wanaofungwa na viwanda vipo ni kuleta cherehani tu mkanunua vitambaa wakashona”-JPM

“Waziri Simbachawene, Mimi kwa sasa ukinikaribisha popote nitakuja kufungua, hata kama ni Jumba la Kuku nitakwenda kulifungua ilimradi limetengenezwa na Magereza kwasababu nimeona mabadiliko, naipongeza Wizara, Kamishna Jenerali wa Magereza Suleiman Mzee na Makamanda wote”-JPM 

“Mmezungumza juu ya upungufu wa Watumishi sasa sijui mnazungumzia Watumishi wa aina gani!, Magereza kila siku mnaajiri, Maaskofu wamo wanaofungwa, Mainjinia, Masheikh, Walimu, Madaktari wapo wanofungwa, mngeweza kuwatumia hao wanaofungwa katika utumishi wenu penye upungufu”-JPM 

“Wafungwa walikuwa hawatumiki vizuri, tunakuwa na Wafungwa wengi, mpaka leo tuna Wafungwa 33,300, nimeenda Isanga(Gerezani) pale pamoja na kusamehe Wafungwa 265 wasinyongwe leo nimekuta Wafungwa wengine 78 wanasubiri niwanyonge, Watu wanapenda kunyongwa”-JPM
#BinagoUPDATES 

No comments