ijue siri kuhusu Sabato(Jmosi) kama siku ya ibada

SWALI - JE AMRI YA PUMZIKO LA SABATO YA SIKU YA SABA, BADO IPO KWA KANISA LA KRISTO SASA?

Imenichukua Miaka mingi tangia nilipopata Kipa Imara katika Kanisa la Moravian na Baadaye Kukua kiroho nikiwa Lutheran, Hatimaye kupokea Wokovu katika Makanisa ya Kipentekoste, KUPATA JIBU SAHIHI JUU YA PUMZIKO LA SIKU YA SABA KAMA AMRI YA MWENYEZI MUNGU INAYOPASWA KUSHIKWA AU LAA.

Nilipata Mafundisho mengi juu ya Uhuru katika Kristo, lakini yakikinzana na Ukweli halisi wa Utii wa Amri za Mungu. Kwa kutumia Mafungu Kama Wakolosai 2:16-17, Warumi 6:14, Wagalatia 3:23, 4:4-5, 5:18 n.k. Nilijihakikishia kuwa niko salama nisipotii AMRI za Mungu, hasa kuwa Pumziko la Sabato halina maana, kwani Sabato ni kuwa ndani ya Kristo.

Pamoja na uhakika huo, Roho Mtakatifu alizidi, kunifunulia maana halisi ya mafungu hayo, na kuniletea maswali yaliyohitaji majibu Kutoka NENO la Mungu, hadi nilipoanza kutafuta kwa makini, majibu ya maswali yafuatayo ndipo nikapata JIBU SAHIHI LA SWALI HILO HAPO JUU ...

Nakualika fuatana nami ili nawe Upanue Maarifa kupitia Uchambuzi huu ... kwa kujibu Maswali yafuatayo ....

1. Kama pumziko la siku moja katika wiki kwa ajili ya kukusanyika na kufanya Ibada, kwa tulio ndani ya Kristo HALIHITAJIKI, Mbona kuna makundi mawili tu? Yaani kundi linalopumzika Jumamosi na Jumapili?  Mbona sioni kundi la wakristo linalopumzika siku nyingine mfano ... Jtano, Jtatu, Alhamisi n.k.? 

2. Je wanafunzi wa Yesu na Kanisa la mwanzo la mitume, wao walikuwa na siku ya Kupumzika na kufanya Ibada? Kama ndiyo ni siku ipi? Kama siyo walifanyeje ili kuwe na utaratibu wa watu wote wawe kwenye Ibada bila wengine kuwa kwenye kazi zao? Je kila mtu alijiamlia siku ya kutokuwa kazini na kushinda kanisani? 

3. Kama kwa mujibu wa Biblia, Mungu aliweka utaratibu wa Pumziko la Sabato ya Siku ya Saba ya wiki? Utaratibu wa Kuanza kukusanyika siku ya Kwanza ... ULIANZA LINI? NA KWA SABABU GANI?

BAADA YA UCHUNGUZI WA KINA WA BIBLIA NA KUREJEA HISTORIA ZA MATUKIO YA UNABII, NILIPATA UKWELI UFUATAO:

1. Siku ya Saba ya wiki ilitengwa rasmi kwa ajili ya Mungu katika wiki ya uumbaji kabla ya anguko la Dhambi - Mwanzo 2:3 .. Akaibariki siku ya saba AKAITAKASA ...", Kutakasa ni kutenga kitu kwa mambo matakatifu ya Mungu ... nikagundua Mungu ni wa utaratibu, akampatia mwanadamu, siku za Kazi na siku moja ya Kupumzika kwa ajili kukutana naye kwa njia ya Ibada. Huo ulikuwa utaratibu wa Mungu EDEN.  Mwenye HEKIMA atakubaliana na hili. 

2. Baada ya Aguko la Dhambi, ni dhahiri wanadamu waliendelea kufuata utaratibu wa Mungu ... hadi waisraeli walipochukuliwa utumwani, ni wazi kule misri hawakuruhusiwa kufanya Ibada, ndio maana walipotolewa utumwani, wakakumbushwa utaratibu wa Mungu ... Kutoka 20:8-11, wakaambiwa "IKUMBUKE siku ya Sabato UITAKASE", Kuitakasa ni KUITENGA KWA MAMBO YA MUNGU ...

SABABU YA KUITAKASA: 
Kutoka 20:11 "Maana kwa siku sita Bwana alifanya Bingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo .... kwa hiyo Bwana AKAIBARIKIA siku ya Sabato AKAITAKASA". Hii ndiyo sababu pekee ya Amri hii. 

3. Katika mafundisho ya Yesu, nikagundua kuwa mafarisayo WALIIHARIFU Sabato, kwa kuitumia vibaya na kuifanya mzingo badala ya kuwa Baraka kama Mungu alivyokusudia ... alifundisha kutenda mema siku ya Sabato ... Marko 3:4-6, Marko 2:27 ... Akairudisha siku ya Saba kuwa siku watu kukutana na Mungu wao, kama ilivyokuwa kwa Amri zingine. 

4. Jambo lingine la kushangaza ni kwamba, WIKI au Juma la siku SABA limetunzwa kimuujiza kwa Kwa sababu ya kuwepo pumziko la siku ya saba tangia uumbaji ... wanazuoni wanakubaliana na hili, wanadamu au wacha Mungu ndio waliotunza na kuipatia dunia hii utaratibu wa Juma la siku 7, mifumo serikali za vizazi na vizazi, zinabadili kalenda za tarehe na miaka lakini sio SIKU ZA WIKI. 

5. Katika vizazi vya vilivyopita, kumekuwepo na Pumziko la siku moja ya wiki tofauti na Jumamosi ... iliyoanzishwa na wapagani wa a bud miungu, hadi Wakati Yesu anazaliwa Ibada kubwa ya Kipagani ilikuwa RUMI wakiabudu JUA katika siku ya Kwanza ya Juma ... wakiita SUN DAY. 

6. Nikiwa natafuta ukweli wa lini Kanisa la Kristo la Agano jipya lilianza kupumzika siku ya Kwanza au Jumapili, nilishangaa kukutana na vitabu vya Kanisa la RUMI, wakieleza jinsi walivyofanya badiliko la kuhamisha utaratibu wa Ibada ya Kikristo kutoka siku ya Saba hadi ya Kwanza. Na TOFAUTI ZILIZOJITOKEZA KWA WALIOSIMAMIA BIBLIA PEKEE NA WARUMI WALIOAMUA KUINGIZA MAPOKEO YA IBADA YA RUMI ILI KUIMARISHA UTAWALA WA KIDINI RUMI. HAPO NDIPO CHANZO CHA R.C. CHURCH. 

7. Nikagundua pia sababu za kuwepo madhehebu ya Protestants ambayo baadaye yakazaa makanisa ya Kiroho, yote yalichomoka, yali protest, yalipinga mafundisho ya Roma yaliyo kinyume na Biblia, hadi sasa yapo kwenye safari ya Matengenezo ... SOMA HISTORIA YA KANISA ... KUANZIA MITUME WALIPOUWAWA ROMA HADI MATENGENEZO ... WAKATI WA MARTIN RUTHER NA WENGINE. 

KWA UFUPI:
UKISOMA UNABII WA UFUNUO na Danieli, Mungu alishatabiri anguko hili la Kiroho chini ya Utawala wa Rumi ila watu, wanajifanya wa kiroho hawataki kujifunza unabii na kuuthibitisha kwa matukio ya Kihistoria na watapotea kwa kukosa maarifa. 

SUN DAY au Siku ya JUA, iliingizwa kwenye ukristo kuwa utaratibu wa kupumzika badala ya siku ya Saba ... na mfalme wa KIRUMI akiwa anatawala dunia ... tarehe 3. 3. 321 AD,  Baada mitume wote kuuwawa kwa kuitetea kweli ya Biblia. Badiliko la siku ya Ibada ni moja tu ya mapokeo, yako mengi ambayo hadi Leo wakristo wengi wameyarithi bila kujua. 

Ukihitaji vitabu vya historia ya Kanisa na vitabu vya R.C vinavyoelezea badiliko hili ... ninanvyo, na vingine vipo KATHEDRO BOOKSHOP, wao wanadai Wamepewa mamlaka ya KUBADILI AMRI za Mungu, yaani wana mamlaka ya KUFUNGA NA KUFUNGUA LOLOTE. 

UFAHAMU HAYA:
1. Kama unaamini kuwa kweli Mungu hana utaratibu wa watu kufanya kazi na siku moja wote wapumzike na kukusanyika kwa ajili ya Mungu, basi endelea, fanya kazi siku zote, na kila mtu aamue siku ya kupumzika anayotaka yeye .... MSIFUATE AMRI YA MFALME WA RUMI YA KUPUMZIKA SIKU YA JUA - SUN DAY. 

2. Kama unaamini kuwa Mungu ni utaratibu katika vizazi vyote, na aliitenga siku ya saba kuwa ni ya kumpa utukufu yeye, kuonyesha kuwa tunayemuabudu ndiye MUNGU MUUMBAJI, basi fuata neno lake, itumie siku ya saba kama Yesu alivyoifundisha. 

3. Kama ilivyokuwa Wakati wa Israeli ndivyo ilivyo sasa, shetani anapiga vita watu wasimpe utukufu Mungu kuwa ndiye Muumbaji, Ibada ya JUA ilianzishwa makusudi na Ibilisi kupinga utaratibu wa Mungu aliouweka kumtukuza yeye, shetani hakubali Cheo cha Mungu cha uumbaji .... kwa HILA NA UMBEMBELEZI NA HATA KWA VITA ... WANADAMU WANAONGOZWA KUMUASI MUNGU. 

#BARIKIWA_SAMBAZIA_WENGINE.

No comments