HISTORIA FUPI YA MAALIM SEIF SHARIF HAMAD
Maalim Seif Sharif Hamad alizaliwa Okotba 22, 1943 na alipitia Shule za Uondwe na Shule ya Wavulana ya Wete kisiwani Pemba kati ya 1950 – 1957.
Sekondari alisomea katika shule ya King George VI Memorial mjini Zanzibar, na aliendelea na masomo ya cheti cha cha sekondari katika shule hiyo.
Alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuanzia 1972 -1975 na kuhitimu na shahada ya sayansi ya siasa, utawala wa umma na mahusiano ya kimataifa.
Amekuwa katika siasa za Zanzibar tangu miaka ya 1970, akiwa mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri wa Elimu kati ya 1977 – 1980, na mjumbe mwazilishi wa baraza la wawakilishi visiwani humo.
Baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini Tanzania mwaka 1992, Hamad pamoja na wanachama wengine wa zamani wa CCM waliunda Chama cha Wananchi CUF.
Machi 2019, Maalim alijiunga na Chama cha ACT Wazalendo ambacho amekuwa nacho mpaka kifo kilipomkuta ambapo amehudumu kama Makamu wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
pumzika #Maalim
#BinagoUPDATES
Post a Comment