GODWIN GONDWE AMETOA MWEZI MMOJA KWA KAMPUNI YA SYNO HYDRO KUWALIPA WAFANYAKAZI MADAI YAO

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh.Godwin Gondwe, ametoa mwezi mmoja kwa kampuni ya Syno Hydro kuwalipa wafanyakazi ambao hawajawalipa madai yao halali wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Tito ni mfano wa wafanyakazi ambao wamekuwakinyanyaswa hapa, mpaka nilipokuja wiki mbili zilizopita ndio mkamlipa. Acheni kunyanyasa wafanyakazi", alisisitiza Mh.Gondwe.

Kwa Upande wa Ujenzi wa  Mradi wa barabara ya Mabasi yaendayo kasi, Mh.Gondwe amekemea kampuni hiyo kufanya ujenzi usio na kiwango.
" Huu ni Mradi wa miaka mitatu, mpaka sasa mwaka mmoja na nusu umepita lakini bado mko asilimia kumi tu( 10%), wakati wenzenu wa kampuni ya CCECC upande wa ujenzi wa vituo vikubwa vya mwendo kasi wako zaidi ya asilimia Sabini( 70%), mlete mpango kazi wenu wa jinsi mtakavyofidia muda uliopotea, pelekeni Tanroad nami nipate nakala," alisisitizz Mh.Gondwe.

"Siwezi kukubali miradi ya kimkakati ya Rais Mh. Dr.John Pombe Magufuli inahujumiwa katika wilaya ninayoiongoza, haiwezekani"  alisema Mh.Gondwe.

Mradi huo unaigharimu serikali bilioni 217.
#BinagoUPDATES

No comments