amka na BWANA
KESHA LA ASUBUHI
Alhamisi 04/02/2021
*MSAADA KATIKA KUJIFUNZA*
*Jitahidi kujionyesha kuwa umekubaliwa na Mungu, mtenda kazi asiye na sababu ya kutahayari, ukitumia kwa halali neno la kweli.* *2Timotheo 2:15*
*Kuwa mwangalifu namna unavyotafsiri Maandiko. Yasome kwa moyo uliofunguliwa kwa ajili ya Neno la Mungu kuingia, nalo litadhihirisha nuru ya mbinguni, na kumtia ufahamu mjinga*. Hii haimaanishi akili dhaifu, bali wale ambao hawapanuki zaidi ya kiwango na uwezo wao katika kujaribu kuwa halisi na wenye kujitegemea katika kuufikia ufahamu ulio juu ambao hufanyiza ufahamu halisi.
*Wote wanaojishughulisha na Neno la Mungu wanashiriki katika kazi muhimu na takatifu sana; kwa kuwa katika utafiti wao watapokea nuru na ufahamu sahihi, ili waweze kuwapatia wale wasio na ufahamu.* Elimu ni kuingiza mawazo ambayo ni nuru na kweli. Yeyote ambaye kwa bidii na uvumilivu huchunguza Maandiko ili aweze kuwaelimisha wengine, akiingia katika kazi kwa usahihi na kwa moyo wa kweli, akiweka kando mawazo yake ya awali, haidhuru yalikuwaje, na athari za urithi katika mlango wa uchunguzi, atapata ufahamu.
Lakini ni rahisi kuweka utafsiri usio sahihi katika Maandiko, kuweka mkazo katika vifungu, na kuvipatia maana, ambayo, katika uchunguzi wa kwanza, inaweza kuwa sahihi, lakini ambayo kwa uchunguzi zaidi, utaonekana usio sahihi. *Ikiwa ni mtafuta kweli atalinganisha Andiko kwa Andiko, atapata ufunguo unaofungua nyumba ya hazina na kumpatia ufahamu wa kweli wa Neno la Mungu.* Kisha ataona kwamba mawazo yake ya awali hayaendani na matokeo ya uchunguzi, na hivyo kuendelea kuyaamini unaweza kuwa ni kuchanganya uongo na ukweli.
*Daudi mtunga Zaburi katika uzoefu wake alikuwa na mabadiliko mengi katika akili yake. Kuna wakati, alipata fikra juu ya mapenzi na njia za Mungu, akainuliwa sana. Kisha alipoona kinyume cha rehema na upendo wa Mungu usiobadilika, kila kitu kilionekana kufunikwa katika wingu la giza. Lakini kupitia katika giza alipata kuona sifa za Mungu, ambazo zilimpa ujasiri na kuimarisha imani yake.*
*Alipokuwa akiomboleza na kuomba, alipata mtazamo halisi wa tabia na sifa za Mungu, kwa kufundishwa na mawakala wa mbinguni, naye aliamua kwamba mawazo yake juu ya haki na ukali wa Mungu vilikuwa vimepotoshwa.*
*TAFAKARI NJEMA MUNGU AKUBARIKI MPENDWA*
Post a Comment