amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
JUMATANO, FEBRUARI, 3, 2021
SOMO: KWA WAOGA, WALIO DHAIFU, NA WANYONGE
Umtumaini BWANA ukatende mema, Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
Zaburi 37:3.
"Umtumaini Bwana," kila siku ina mizigo yake, masumbufu yake, na fadhaa zake; na tunapokutana, tuko tayari kiasi gani kuzungumza kuhusu magumu na majaribu yetu. Matatizo mengi ya kujitafutia huingilia, hofu nyingi huendekezwa, mzigo wa wasiwasi huoneshwa, kiasi kwamba karibia mtu adhani kwamba hatuna Mwokozi mwenye huruma na upendo, aliye tayari kusikia maombi yetu yote na kuwa kwetu msaada ulio karibu wakati wa hitaji.
Baadhi ya watu mara nyingi ni wenye hofu na kujitafutia fadhaa. Kila siku wanazungukwa na ishara ya upendo wa Mungu, kila siku wanafurahia wingi wa majaliwa yake; lakini hawatilii maanani baraka hizi za sasa. Akili zao mara zote hufikiri sana juu ya kitu tofauti ambacho wanaogopa kinaweza kutokea; au kwamba ugumu fulani kwa hakika waweza kuwepo, ambao, japo ni mdogo, huwapofusha macho yao kwa mambo mengi yanayohitaji washukuru. Magumu wanayokutana nayo, badala ya kuwapeleka kwa Mungu, chanzo pekee cha msaada, huwatenga naye, kwa kuwa wanaamsha misukosuko na kuona uchungu.
Ndugu na dada, je, tunafanya vyema kwa kutokuamini? Kwa nini tunakosa shukrani na kukosa kutumaini? Yesu ni Rafiki yetu. Mbingu yote inapendezwa na ustawi wetu; na wasiwasi na hofu yetu humhuzunisha Roho Mtakatifu wa Mungu. Hatupaswi kuendekeza mambo ambayo hutuletea mashaka na kutuchosha, lakini hayatusaidii kustahimili majaribu. Hakuna nafasi inapaswa kutolewa kwa kutokumtumaini Mungu inayotuongoza kufanya maandalizi kinyume na hitaji la utafutaji mkuu wa maisha ya baadaye, kana kwamba furaha yetu hutokana na hivi vitu vya duniani, na kwamba tungeweza kuvipata huku tukipuuza ukweli kwamba Mungu ndiye mtawala wa vyote.
Unaweza kufedheheshwa katika biashara; matarajio yako yanaweza kuwa katika giza kubwa, na unaweza kutishwa na hasara. Lakini usikatishwe tamaa; mtwike Mungu fadhaha zako, na ubaki mtulivu na mchangamfu. Anza kila siku kwa maombi ya dhati, pasipo kusahau kutoa sifa na kushukuru. Omba kwa ajili ya hekima ili kuendesha mambo yako kwa busara, na hivyo kuzuia hasara na baa. Fanya yote uwezayo kwa sehemu yako ili kuleta matokeo yenye manufaa. Yesu ameahidi msaada wa kiungu, lakini si pasipo juhudi za kibinadamu.
Post a Comment