amka na BWANA leo 21

KESHA LA ASUBUHI

JUMATATU, FEBRUARI, 22, 2021
SOMO: POPOTE, BWANA 

Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. 

Wafilipi 4:11.



Mawazo yamekaza moyoni mwangu kwamba kwa vile sina badiliko katika afya yangu ya kimwili si vizuri sana kusimulia maumivu yangu au saa zangu za kukosa usingizi wakati wa usiku. Kwa hiyo siku baada ya siku inapita na uzoefu wangu ni ule ule. Mwili wangu umejaa maumivu ya viungo. Sina hamu wala furaha ya kula, na wakati ninapokaa kwa muda mfupi ni hatua zenye maumivu makali sana kuinuka. Miguu yangu hukataa kutii kutaka kwangu, na nikisogeza tu ninapata maumivu makali sana. 



Nina mawazo mengi sana kwamba sikutumwa katika nchi hii [Australia] kwa mapenzi ya Bwana. Kuna wakati nahisi uthibitisho kwamba mapenzi ya Mungu kwangu yalikuwa mimi kubakia California, nyumbani kwangu mwenyewe, na kuandika kwa kadiri niwezavyo Juu ya maisha ya Kristo. Nina hakika juu ya jambo moja —kwamba watu wanahitaji msaada katika nchi hii. Na niliogopa ungekuwa ni ubinafsi, au kutafuta raha, kukataa kwenda Australia. 



Kwa kipindi cha maisha yangu nimejaribu kufanya kile ambacho kilipingana na matakwa yangu kwa sababu Kristo kielelezo chetu hakuishi kwa kujipendeza yeye mwenyewe. Kwa kurudia rudia, kwa gharama kubwa, nimewaza kwamba ningejipatia sehemu ya kwenda na kupumzika, ambapo ningeweza kuandika juu ya maisha ya Kristo, wakati baadhi ya miito ya dhati ilipokuja toka mahali ambapo msaada ulihitajika, na ombi likafanywa ili kutoa ushuhuda wangu miongoni mwa makanisa. Sikuthubutu kusema hapana. Mara moja niliitikia kwamba ningefanya kwa kadiri ya nguvu ambazo Bwana angenipa. Baada ya kazi hii kumalizika katika udhaifu wangu, kisha majukumu mengine huko Battle Creek yalihitaji kufanyiwa kazi ambayo yalinihitaji kubeba mzigo mchana na usiku, na kuwa katika maombi mengi katika masaa ya usiku ambapo nisingeweza kulala. 



Niliposafiri kwenda California niliamini kwa_ hakika kuwa ningebakia huko kwa kipindi chote cha majira ya baridi, lakini wengi walitoa mawazo yao kwamba sasa ni wakati wa kwenda Australia. Sikuweza kutulia, bali nilienda, kulingana na sauti na nuru ya ndugu zangu. Sasa nilipokuja Australia mzigo ulikuja juu yangu na nilifanya kazi kama nilivyofanya hata sasa. 



No comments