amka na Bwana leo 14

*KESHA LA ASUBUHI*

Jumapili, 14/02/2021

*WATENDA KAZI PAMOJA NA MUNGU*

*Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu, ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu*. 
*1 Wakorintho 3:9.*

Watie moyo wale ambao kwa ajili yao Kristo ameyatoa maisha yake. Waongoze kuelewa kuwa hawapaswi kuyategemea mazingira yao kwa ajili ya uzoefu wa Ukristo wao. Itakugharimu jitihada kuwafanya watambue jukumu lao la kuwa wafanya kazi pamoja na Mungu. Lakini zingatia kuwa Kristo, katika kipindi cha miaka ya utume wake duniani, aliteseka siku zote, na mara nyingi bila mafanikio. 

Waoneshe watu hasara ya milele ambayo watapata wale wanaokataa kutoa moyo, na akili na nafsi kwa ukamilifu kwa Kristo. *Kila siku inayopita ambayo Yesu ananyimwa ukubali wa kuingia moyoni, ni siku iliyopotezwa*. Kisha waoneshe wale ambao kwa ajili yao unatenda kazi ni kwa kiasi gani ilivyo na manufaa kujisalimisha kwa Mungu. 

*Maombi humpatia mtenda kazi kwa ajili ya Mungu nguvu ya kiroho kuanza tena upya mapambano. Hiki ndicho chanzo cha nguvu yako kubwa kabisa. Mungu huoneshwa kama anayeinama kutoka mahali pake mbinguni, akiwatazama kwa shauku iliyo hai wale wanaomtendea kazi, akiwa tayari kuwapatia neema wale wanaosihi katika kiti chake cha enzi*. 

*Kamwe usisahau kwamba wewe ni mtendakazi pamoja na Mungu*, na kwamba ni fursa yako kulindwa kwa uthabiti na neema yake. *Kristo hutazama kwa shauku kila tendo la matengenezo linalofanywa duniani. Anamtaka kila mmoja alitajaye jina lake kuongoka kila siku, ili aweze kutenda kwa weledi katika kazi yake, chini ya uongozi na uwezo wa Roho Mtakatifu*. 

*Ni kusudi la Mungu kwamba watu wake wawe waliotakaswa, waliosafishwa, watu watakatifu, wanaotangaza nuru kwa wote wanaowazunguka. Lakini tu ni kwa kadiri watakavyodumisha kiwango juu, ikiwa tu watadhihirisha kwamba kweli wanayokiri kuiamini inaweza kuwavuta kuwa wenye haki na kutegemeza maisha yao ya kiroho; ikiwa tu watafanya kanuni za kweli kuwa sehemu ya maisha yao ya kila siku, ndipo wanaweza kuwa sifa na heshima kwa Mungu duniani. Ni fadhila ya kila Mkristo kupokea neema ili kumwezesha kusimama imara kwa kanuni za haki katika utumishi wa Mungu.*

*MUNGU ATUBARIKI TUNAPOTAFAKARI NENO LAKE*

No comments