ZITTO KABWE AWASIHI WATU KUWA MAKINI, NIMONIA MPYA NI NOMA

"Namsihi Waziri wa Afya, Dkt. Dorothy Gwajima, ambaye kitaaluma ni daktari atoe ufafanuzi kwa  Umma 

- tofauti ya Nimonia hii nchini na Covid 19 duniani,
- Dalili zake na namna ya kujikinga;na 
- Idadi ya wagonjwa na vifo mpaka sasa na maeneo gani ya nchi"

Inaonekana tuna Nimonia ya kipekee nchini. Nawashauri Watanzania 
- Tunawe mikono kwa maji tiririka, 
- Tuepuke kupiga chafya bila kujifunika 
- Usisite kwenda hospitali ikiwa unahisi una dalili za mafua makali, homa na kuchoka mwili.

Usichukulie poa, nimonia mpya ni noma" - Zitto Kabwe#BinagoUPDATES

No comments