WASAFIRI WA MABASI KUANZA KUPIMWA COVID-19
TANZANIA:WASAFIRI KUPIMWA COVID-19 KWA TAKRIBAN TSH. 230,000;"
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa muongozo mpya wa upimaji kwa wanaosafiri kwenda nje ya nchi kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanaoambukizwa CoronaVirus na kuwepo kwa vimelea vipya kwa baadhi ya nchi"
Wizara imetangaza kupanda kwa gharama za upimaji wakisema kuwa zimechangiwa na ongezeko la wasafiri wanaokwenda nje ya nchi na mabadiliko ya teknolojia ya upimaji ambapo baadhi ya vipimo vimeongezeka"
Muongozo unataka msafiri aelimishwe siku tano kabla ya siku ya Safari. Aidha, Vyeti vya Kielektroniki vya COVID19 vitatolewa kwa waliothibitika kutokuwa na maambukizi na vitadumu kwa siku 14 au kutegemea na nchi ambayo msafiri anakwenda"
Majibu yatatolewa ndani ya saa 48 kabla ya safari kwa watu wa nje ya Dar es Salaam na ndani ya saa 24 kwa walioko mkoa wa Dar. Gharama za Vipimo ni USD 100 sawa na Takriban Tsh. 230,000 ambapo malipo yatalipwa katika Akaunti ya Serikali."
Post a Comment