TAMMY ABRAHAM AMTETEA ANTONIO RUDIGER JUU YAKUFUKUZWA KWA LAMPARD

Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Tammy Abraham amemtetea mchezaji mwenzake wa timu hiyo Antonio Rudiger ambaye ameshutumiwa vikali na mashabiki kuwa ndiye aliyechochea Frank Lampard kutimuliwa klabuni hapo. 

Ripoti zinadai kuwa Rudiger ni mmoja ya waliokuwa wakisababisha kutokuwepo kwa utulivu katika vyumba vya kubadilishia nguo, wengine ni Marcos Alonso na Jorginho. 
Pia Rudiger ameripotiwa kugombana na nahodha Cesar Azpilicueta zaidi ya mara moja katika utawala wa Lampard. 

“Ninasikia vitu fulani vya kijinga kuhusu Rudiger katika mitandao ya kijamii leo. Upuuzi kabisa. Toni ni kaka yetu mkubwa kwetu sisi wote.” — Aliandika Tammy kwenye kurasa yake ya Twitter na kuungwa mkono na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Didier Drogba ambaye alisema : “Umeongea vizuri, Hii ndio njia. Kaeni pamoja, pateni matokeo na mashabiki watawasamehe kila kitu.”

“Wakosoaji wanaumiza lakini mnapokuwa pamoja inawafanya imara na bora”
#BinagoUPDATES

No comments