JPM; HAKUNA CHAKULA CHA BURE
“Sitatoa chakula kwenye Wilaya yoyote, hakuna chakula cha bure kama mlivyozoea huko nyuma, Mimi usipofanya kazi usile na usipokula kufa, lazima tuambiane ukweli, Watu wafanye kazi, walime, na asiyefanya kazi asile,
Sitatoa chakula katika Wilaya yoyote, na Wilaya itakayopata njaa DC ataondoka na Viongozi wengine wanaostahili kuhamasisha Wananchi kufanya kazi wataondoka, tunataka pesa tunayopata ifanye kazi nyingine, tunatoa Elimu bure, tunajenga SGR ndio kazi za Serikali, sio kukulisha” -Rais Dkt John Pombe alipokuwa akizungumza mbele ya Wananchi wa Bahi mapema leo akitoka Tabora kuelekea jijini Dodoma.
#BinagoUPDATES
Post a Comment