amka na Bwana leo 30

KESHA LA ASUBUHI

Jumamosi 30/01/2021

*TATIZO LAKO LINA UFUMBUZI*

*Lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.* *Isaya 66:2*

Uliletwa mbele yangu kama aliye na mashaka na kukata tamaa. Yesu alisema juu yako kama alivyosema kwa Petro, *“Shetani amewataka ninyi apate kuwapepeta kama vile ngano; lakini nimekuombea wewe ili imani yako isitindike, (Luka 22:31,32). *Ninakuletea Habari njema; Yesu anakupenda, wewe uliyekumbwa na dhoruba. Imani yako haijavunjika, ingawa Shetani amejaribu kukufanya uamini kwamba imevunjika. *Tazama na uishi. Njoo kwa Kristo jinsi ulivyo. Mpokee kama Mwokozi wako binafsi.* 

Umetenda makosa, lakini si kwa kukusudia; ulivutwa mbali na majaribu. Umiliki wa mali nyingi ulilewesha akili yako na kupotosha uamuzi wako. Hukutambua namna ya kutumia mali kwa hekima, kwa utukufu wa Mungu. Hata hivyo, bado umewekeza mali katika kazi yake, na mahali ambapo itatumika kwa utukufu wake. Ndugu yangu, japokuwa haukudhihirisha hekima yote ambayo ungepaswa na kukulazimu kutumia, Mungu amekubali yote uliyofanya ukiwa na shauku ya kutangaza utukufu wake.

Maneno haya nilipewa kwa ajili yako: *“Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema,mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake” (Waebrania 2:17)*, kupitia upatanisho. Mwenye dhambi anayetubu anapaswa kumwamini Kristo kama mwokozi wake binafsi. Hili ndilo tumaini lake pekee. Anaweza kushikilia ustahilifu wa damu ya Kristo, akipeleka kwa Mungu Mwokozi aliyesulibiwa na kufufuka kama kustahili kwake. Hivyo kupitia kwa sadaka ya Kristo ya kujitoa mwenyewe, asiye na hatia kwa aliye na hatia, kila kikwazo kimeondolewa, na upendo wa Mungu unaosamehe hutiririka katika mito ya rehema kwenda kwa mwanadamu aliyeanguka... 

*Njoo tu kwa Yesu sasa, ikingali leo. Uzoefu ambao umekuwa ukiupitia utathibitisha kuwa wa thamani kuu utakapojifunga nira na Kristo, kuwa mtenda kazi pamoja na Mungu. *Umejifurahisha katika kweli, umeiamini kweli, na bado unaiamini, na tumaini baada ya tumaini kwa kuwa Roho Mtakatifu anapambana pamoja nawe* 

*Umetengeneza njia zilizopotoka kwa ajili ya miguu yako kwa sababu ya majaribu, bali mpinge mwovu, naye atakukimbia; mkaribie Mungu, naye atakukaribia.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA MPENDWA*

No comments