MOYO WA MWANADAMU

*MOYO WA MWANADAMU* 
Bwana Yesu Asifiwe! Leo nimekueletea somo hili litakalo kusaidia sana.kwani watu wengi tunazungumzia habari ya moyo bila ya kufahamu siri iliyoko ndani ya mioyo yetu.

Muhimu kujua neno moyo limeandikwa mara 581, na Moyo Kibiblia haina maana ya wazi ya kuonesha kuwa ni kiungo cha mwili kinacho sukuma damu kwenda kwenye sehemu nyingine za mwili, bali ,moyo huo unasifa zifuatazo;
 *#Kutumaini* ; (Mithali 3:5), Kuoshwa na kuwa safi (Yeremia 4:14 & Mathayo 5:8), Makao ya NENO la Mungu ambapo huyu NENO ni MUNGU na pia ni Madhabahu ya BWANA YESU (Yohana 1;1-4 & Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11), Moyo unapaswa kulindwa; (Mithali 4:23 KJV), Moyo unaongea; ( Mwanzo 8:21), Moyo ni mdanganyifu *( Yeremia 17:9)* 

Unapoona moyo unasifa za namna hii la hasha lazima utajiuliza kuwa ni moyo wa namna gani huo? Na ndipo utagundua moyo unaozungumziwa hapa, sio moyo wa kusukuma damu, bali moyo huu ni Nafsi iliyohai na itambulike hata Mungu ana_moyo pia.
 *Mwanzo 8:21 KJV* 
[21] BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; *BWANA akasema moyoni,* Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, *maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake;* wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya.

 *Hata hivyo,* Binadamu wenyewe tumeshindwa kuielewa mioyo yetu wenyewe, lakini Mungu anaielewa, kwa kawaida  moyo  ni kama fumbo lililo fumbwa na mwenye ufumbuzi wa moyo ni Mungu, 
 *Yeremia 17: 9 KJV*  Biblia inasema, 
"Moyo huwa mdanganyifu kuliko vitu vyote, una ugonjwa wa kufisha; nani awezaye kuujua?" 
 *Zaburi 44:21 KJV* 
[21] Je! Mungu hatalichunguza neno hilo? Maana ndiye azijuaye siri za moyo.

 *Lakini pia,* Mungu anachunguza mioyo, na kumpa mtu alivyo navyo kwa kuiangalia mioyo, hivyo hapa unaanza kuona Mungu hampi chochote aombacho bali humpatia kwa kuiangalia mioyo yetu,  kwanini kwasababu moyo ni fumbo, kuna eneo dogo sana la mtu kuujua moyo wake kuliko vile Mungu atujuavyo.
 *Yeremia 17:10 KJV* 
[10] Mimi, BWANA, nauchunguza moyo, navijaribu viuno, *hata kumpa kila mtu kiasi cha njia zake, kiasi cha matunda ya matendo yake.* 

*Kwasababu hiyo* wanadamu hatuna budi kuomba wakati wote kuumbiwa moyo safi, moyo wa ibada wenye unyenyekevu, uliopondeka na wenye kujali watu ambao kwaasili moyo safi ndio moyo halisia wa Mungu ambao hapana mtu atakaye mwona Mungu bila ya huo moyo safi, na leo mioyo tuliyonayo ni mioyo ya kisasi, husuda, jeuri, kiburi, na kadhalika.
 *Zaburi 51:10 KJV* 
[10] Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
 *Ezekieli 36:26 KJV* 
[26] Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, *nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu,* nami nitawapa moyo wa nyama.

 *#Ni rahisi sana kwa nje* kumwona mtu mwema bila kujua yaliyo ujaza moyo wake, kuna watu wengi tunapenda kujihesabia haki na kuwaona wengine hawafai, hawawezi, hawatafika mbali bila ya kujua hali ya moyo huu sio moyo wa Mungu na kwa hakika tunahitaji Mungu aingilie kati kutusaidia sana eneo la kuutengeneza moyo, fikiria mtu unayecheka naye, unayeishi naye si ajabu ni kiongozi au ndugu wa karibu sana ukagundua ndio adui yako anaye kuroga anayepanga njama za kuuawa kwako, leo hii vijana wengi na ndoa nyingi zinasumbua kwasababu ya uharibifu wa moyo, kuna watu wamekata tama ya kuabudu, kusali, kusaidia watu kwasababu mioyo yao imeharibiwa na kujeruhiwa sana, kuna watu leo wamekata tama ya kuishi, kuoa au kuolewa kwasababu mioyo yao imeharibiwa, ndio maana Biblia ikasema;
 *Mark 7:21-23 SRUV* 
[21-23] Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi. 
 *Mithali 4:23 KJV* 
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. 
Ni maombi yangu Mungu akuponye na aniponye moyo wangu

*UKIRI* 
Ee Mungu, naomba nisamehe kwa kukosea na kuwakosea watu wengi kutokana na moyo wangu ulivyo, nisamehe kuwawazia wengine mabaya nisijue mawazo yako kwetu ni mema nay a kutupa tumaini siku zetu zote za  maisha, naomba niumbie moyo safi, moyo wa ibada, moyo wa kuomba, moyo wa uaminifu, moyoi ulioepukana na mabaya kwa Jina la Yesu. (Chukua dakika chache omba juu ya moyo wako kuendeleza maombi niliyo kuongoza) 
COMMENT: *MUNGU NIUMBIE MOYO SAFI, MOYO MPYA , MOYO WA IBADA nk* 

 *(NB)* Kama unaona Mungu amesema nawe eneo la Moyo, na unaona kuna eneo moyo wako umejeruhuika kiasi kwamba umefikia hatua mbaya ya mahusino yako na Mungu na watu, umeona kiu ya kuomba, kuoa au kuolewa imeondoka, kusaidia watu na majeraha mengine makubwa tafadhari wasiliana nami kupitia;
 *Whatssapp No:*  0765830426
 *SMS & Calls:*        0657076518
 *Email:* elishasaimoney@gmail.com
 *Shepherdelisha_international_Ministry*
#BreakingNews #BinagoUpdates #MAHUBIRI

No comments