Usiyachochee Mapenzi ktk umri mdogo
KWA NINI KUYACHOCHEA NA KUYAAMSHA MAPENZI KABLA YA WAKATI WAKE??
Nawasalim watu wote katika Jina la YESU KRISTO.
Natumaini kila mmoja ni mzima wa afya, hata wale ambao hali zao kiafya hazipo vyema ni matumaini yangu kuwa MUNGU wa mbinguni ataachilia uponyaji.
Leo nimepata msukumo mkubwa kuzungumzia mada tajwa hapo juu.
Watu wengi sana wamejikuta wakimtenda MUNGU Dhambi kwa kujitoa ufahamu katika NGONO.
~Wimbo Ulio Bora 2:7
"Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe."
-Leo kumekuwa na ongezeko kubwa la watu wengi kutumbukia katika UZINZI na UASHARATI kwa kujiendekeza.
>Ni muhimu kutambua kuwa hakuna bahati mbaya katika kuzini/Uasherati maana ni kitendo kinachofanyika mtu mwenyewe akiamu kutenda uovu huo.
-Yapo mambo mtu huyafanya kama masihara kumbe tayari anajitumbukiza katika UOVU wenyewe. Kila jambo ili lifanyike lazima kuandaliwe mazungira ambayo yataruhusu jambo lile kutendeka kwa ufasaha zaidi.
>Yafuatayo ni mambo ambayo ukiyafanya tambua unayachokoza mapenzi au hisia kuamka. Hapa ni muhimu kutambua kuwa simzungumzii Mke na Mume; Bali ni watu ambao si wanandoa.
1: CHARTING KWA NJIA YA SIMU.
Mawasiliano kwa njia ya simu huweza kuchochea kuamka kwa Hisia za mapenzi.
Watu wengi katika kipengele hiki, wanajikuta tayari wamekwisha kuzini hata kwa mafikirio tu.
Haiingii akili mtu kuwasiliana na mtu jinsia tofauti na wewe halafu unatumia vijimaneno kama vya mume na mke.
Yapo maneno ambayo hutumiwa huleta hisia chafu kwa watu wengi.
Mfano, Ni saa za usiku; Kijana anamtafuta Binti either kwa sms au voice call, anaanza kumuuliza umelalaje? Au umevaa nguo gani? Au anamwambia nipetipeti maana nimekumis!! Sasa unategemea nini kitakachofuata katika Charting hiyo!?
Ni muhimu kuepukana na mazingira kama hayo kama kweli unahitaji Kuupendeza Moyo wa Mungu.
2-MAONGEZI/MAZUNGUMZO MABAYA:
Mara zote maongezi mabaya huharibu tabia njema kwa watu wengi sana.
1 Wakorintho 15:33-34
[33]Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.
[34]Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.
-Wimbi kubwa la watu huona kama maongezi yote yanafaa kwa kila mtu kumbe sivyo. Lazima hata mazungumzo yawe na mipaka yako.
Wewe ambaye si mwanandoa, acha kabisa kuwasha moto mahala ambapo sio pa kuwasha moto huo.
Kila mtu anapaswa auwashe moto wa mapenzi kwa mwenzi wake wa Ndoa na si vinginevyo.
Mazoea, Masihara, Utani utani, huchochea roho ya uasi.
Ukitambua kuwa wewe ni wa thamani acha kabisa kumkosea MUNGU.
JENGA mazingira ambayo hayakutii katika kuchochea Hisia.
Usikubali kama wewe ni Mwanaume kujaza picha za mabinti ambao unajua kabisa huna unasaba wowote maana utaanza kuingiwa na kiroho kichafu.
Usipende kujirahisisha kwa jinsia tofauti inaweza kukuangamiza kiroho.
Ni wazi kuwa lazima umhitaji Roho Mtakatifu yeye abadili mtazamo Wako wa fikra.
Kama unatambua ya kuwa unaendelea kumwasi Mungu kwa namna yoyote ile, huna budi utubu. Toba ya kweli huleta uzima wa milele kwa kumuamini YESU KRISTO, Ya kuwa ni Bwana na Mwokozi wako.
ASANTE.
The Light Of Universe Ministry
Mwl Ejide Andrew Noah
+255743154575.
Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv
Post a Comment