upendo

•••••••••••NENO LA FARAJA••••••••••••••••••
💞HAKIKISHA NYUMBANI HAKUNA UNYANYASAJI💞
_______________________________________
Upendo ukitawala familia inahimarika na kuwa sawa kila nyanja ya maisha ....!
Waefeso 5:1-2
📯Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa;
📯mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.
📯Taswira hapa ni kuwa na upendo unaofanana na wa Yesu. Upendo wa kujitoa kufa kwa ajili ya marafiki zako, na watu wote.
📯Upendo unaoakisi uharisia wa maisha ya Yesu Kristo. Chimbuko la upendo huu ni pale Calvary (msalabani) ....huu hutuvuta kupendana sisi kwa sisi. Kwa mjibu huo hatuta kuwa na unyanyasaji ktk familia zetu.
📯TAZAMA HII📯
Waefeso 5:28-29
❤️Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
❤️Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.
_____Kila mfumo wetu wa maisha unapaswa kuwa na upendo kama vile Kristo alivyo lipenda kanisa.(ndoa).
❤️UTII KTK NDOA NI MOJA YA TUNDA LA UPENDO ❤️
Waefeso 5:22-25
📯Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
📯Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
📯Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
📯Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;
❤️WATOTO ❤️
Waefeso 6:1-4
📯Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
📯Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
📯Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia.
📯Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.
❤️Amri ya kuwaheshimu wazazi ni amri yenye AHADI ndani ake na ina mibaraka tele kwa watoto.(Amri ya 5). Tunapaswa kuwaheshimu watu wote hata wadogo kwa wakubwa......haswa walio juu ya umri wetu.
❤️ Unyanyasaji hautakuwepo katika ndoa au familia kama UPENDO, HESHIMA, UTII NA UPOLE vitaangaza ndani ya nyumba zetu bila kumnyanyasa mtu yeyote......!
❤️Ikiwa baba au mama unavaa vizuri, unakula vizuri na huwajali watoto huko ni kuwanyanyasa. 
 ❤️Kumbuka familia bora ndiyo inayoleta kanisa lenye washiriki bora. Na hii ndiyo halisi ya tabia ya Yesu Kristo. 
____Barikiweni_____

No comments