sema Ameni,Mungu yupo

*KWA WOTE WANAO SUBILI MAJIBU YA MAOMBI YAO TOKA KWA MUNGU* .

Tembo na mbwa walishika mimba kwa wakati mmoja. miezi mitatu baadae mbwa alizaa watoto sita. 

baada ya miezi sita mbwa alibeba tena mimba nyingine, na ilipofika miezi tisa alizaa watoto wengine kumi na wawili  

Miezi kumi na nane baadae mbwa aliamua kumfuata tembo na kumuuliza "unahakika kwamba kweli una mimba"? Maana sote tulibeba mimba wakati mmoja, mm nimesha zaa mara mbili mpaka sasa nina watoto zaidi ya dazani lakin ww bado una mimba ileile tu, nn kinaendelea?

Tembo akajibu "kitu kimoja ambacho inakupasa utambue ni kwamba nilie mbeba tumboni mwangu sio mbwa bali ni tembo. AkaendeIea huku akisema ninazaa mara moja tu ndani ya miaka miwili,  lakin siku nikimshusha mwanagu ardhini dunia lazima ihisi kitu, na pindi mwanangu anapokatiza barabarani,binadam husimama na kusitisha shughul zao hivyo bas nilicho beba kina thamani kubwa sana."

 *FUNZO* 
Usipoteze imani yako unapoona watu wengine wanajibiwa maombi yao, wala usivunjike moyo kama bado hujapokea baraka zako toka kwa Bwana.

Sema na moyo wako kwamba"siku yangu ya kupokea baraka zangu inakuja, Amini Bwana hachelewi wala hakawii, punde Bwana atajibu maombi yako na kwa hakika utaishangaza dunia."

              *SEMA AMINA*
🙏🏻🙏🙏🏻🙏

No comments