nitakuoa

TUFANYE, NINAKUPENDA NITAKUOA.

Wanaume wengi hususani Vijana wamekuwa walaghai katika hisia kwa mabinti kwa kuwahidia ahadi nyingi ili kufanikisha mchezo.

Wanaume wengi wamekuwa wakitumia neno NITAKUOA, ili kuwapata mabinti wengi hata waliopo makanisani.

Wanatumia neno hilo baada ya kuona KIU ya Mabinti wengi wanahitaji KUOLEWA.

Mwanaume humfuata Binti na kumshawishi(KUMTONGOZA) ili kujenga nae mahusiano kwa mgongo kuwa nitakuoa. 

Hatimae Binti husadiki yale maneno na kuamua kuingia katika mahusiano  na mwanaume aliyemsikiliza kuwa Anampenda akiamini kuwa ana MALENGO MEMA.

Baada ya siku mambo huenda tofauti kwa mwanaume kuanza kutaka KULA FAIDA kabla ya KUWEKA MTAJI KATIKA BIASHARA.

Mwanaume anamweleza Binti TUFANYE MAPENZI maana wewe ndio Mke wangu, Binti asiye na Yesu anaona bora amridhishe mwanaume kwa KUMVULIA CHUPI akiamini ataolewa nae.

Mwanaume anafanikiwa kutenda NGONO na Binti, Baada ya Mda mwanaume anaanza visa visa maana Lengo lake ilikuwa kuonja Radha ya Chakula na sio Kumiliki Chakula.

NISIKILIZE E BINTI.
Acha mara moja kuugeuza mwili wako kama kiwanja cha mazoezi.

Unaporuhusu kuvuliwa chupi na kila mwanaume unajiondolea Baraka zako katika maisha yako.

Mwanaume muoaji hawezi kukueleza habari za kumtenda Mungu Dhambi Kamwe. Anayekupenda Atakusihi uwe mwaminifu mbele za Mungu.

ENYI WANAUME
Acheni ushetani kuharibu wake za watu wa Baadae, Usimlaghai Binti ili upate kumchafua na kumwacha.

IVI UNAJUA UNAYEMCHEZEA LEO NI MKE WA MTU MWINGINE??

IVI UNAJUA HATA MKEO ANACHEZEWA NA WANAUME WENGINE??

EWE BINTI UNAJUA KUMVULIA CHUPI KILA ANAYEKUJA MBELE YAKO NI ISHARA HUTAWEZA KUWA MKE MWEMA??

Jitunze ili uwe utukufu kwa Mungu.

No comments