Maana ya Neno R.I.P

R.I.P. NA UMAANA WAKE HALISIA 

📩Tuanzie nyuma kidogo kabla dhambi kuanza, shetani alianza kusema maneno kinyume na maneno ya Mungu kuhusu KIFO, Mungu alitoa onyo kuwa kama mwanadamu angevunja amri ya kula tunda alilokatazwa "Utakufa hakika."  MWANZO2:17 lakini shetani kwa kutumia hila zake akamdanganya mwanadamu na kusema kinyume na Mungu kuwa wakivunja ile amri na kula tunda ''hakika hamtakufa". MWANZO3:4
📩 Kati ya hizi pande mbili yaani upande wa Mungu na wa shetani sote tunajua kuwa upande uliokuwa sahihi n upande wa Mungu maana mwanadamu alipokula tunda ilikuwa ni mwanzo wa kifo tofauti na shetani alivyodanganya kuwa hatutakufa. 
📩Baada ya shetani kufanikisha lengo lake la awali la kutuletea kifo,  amedumu kwa miaka mingi na kuendeleza hila zilezile kuwa mtu hafi japo ni wazi kuwa kila mmoja wetu anajionea kuwa tunakufa ila kwa sasa shetani amedumisha hayo madai kwa namna na njia ya tofauti na makini na kisasa zaidi ambayo ni kuaminisha kuwa "....mtu akifa hafi bali anaenda mbinguni na wengine wanaenda motoni kuteseka kama mtu alikuwa mdhambi au alifia dhambini".
📩Kulingana na Neno la Bwana, mtu akifa hajui lolote wala hatambui lolote "Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa, lakini wafu hawajui neno lolote wala hawana ijara tena maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Mapenzi yao na machukio yao, na husuda yao imepotea yote pamoja, wala hawana sehemu tena katika jambo lolote linalofanyika chini ya jua."  MHUBIRI9:5-6 wala amna chochote kinachoweza kufanyika ili kubadilisha historia yake ya upande aliofia either kama n wa dhambi au wema mana Mungu anatoa onyo na kueleza hili wazi kuwa  "Na kama watu walivyowekewa kufa mara moja,  na baada ya kufa  HUKUMU". Waebrania9:27.
 📩Hukumu inayozungumzwa hapa ni sio hiyo ambayo shetani anadai kuwa kuna kwenda mbinguni au motoni punde tu mtu anapokufa bali neno hukumu linaloongelewa hapa ni kama MHURI, yaani unapokufa tu Mhuri unagongwa kuwa wewe ni wa shetan au ni Mungu na hakuna yeyote wala chochote kinachoweza kufanyika au kufanya au kufanywa ili kubadili upande ambao mhuri umegongwa ulipofia yani kama n dhambini au ni kwa Mungu basi itabaki hvohvo hadi siku ya mwisho ambapo ndipo siku rasimi ya hukumu. 
📩Kwa Mfano Musa alipofariki Mungu aligonga mhuri kuwa ni wa kwake  lakini shetan akataka kudai kuwa ni wa kwake ili mhuri ama hukumu ambayo Mungu alikuwa amepitisha ibadilike hatimaye "Lakini Mikaeli, malaika mkuu aliposhindana na Ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu bali alisema Bwana na akukemee." Yuda1:9 na mwishowe Mungu alishinda hatimaye Mungu  alimfufua Musa na kumpeleka mbinguni ili kuuhakikishia ulimwengu kuwa hukumu ya Mungu asemapo na kuamua haibadiliki kamwe kama ilivyodhihirika kuwa Musa yupo mbinguni pale alipomtokea Yesu akiwa na wanafunzi wake kwenye Marko9:4 inaposema "Wakatokewa na Eliya pamoja na Musa, nao walikuwa wakizungumza na Yesu"

TWENDE SASA KWENYE KIINI CHA MAADA YA R.I.P.
📩Hili neno "R.I.P." ni kifupi cha maneno yanayomanisha "REST IN PEACE"  yaani "PUNZIKA KWA AMANI'
📩Ni maneno yalobuniwa kistadi sana na umakini mkubwa na ibilisi kumaanisha kuwa mtu akifa haijalishi kafia upande gani lakin kwa kusema maneno hayo na mengineyo kama vile "raha ya milele umpatie,  hakika tutakukumbuka, mbele yetu nyuma yako" na mengineyo mengi yanakuwa yanasemwa kwa  mtu aliyekufa yanakuwa na malengo yafuatayo: -

1. Ni kuendeleza madai ya shetani kuwa mtu hafi,  maana mfano unaposema "mbele yetu nyuma yako au punzika kwa amani" huonyesha unaamini kuwa huyo mfu anakuskia na inakuwa ni kama unamfariji asijiskie vibaya kutangulia kufa maana sisi tulio hai tupo nyuma yake tunakuja kumfuata.  Kwa kusema maneno hayo pengine bila kujua hujikuta mtu amekua upande wa ibilisi aliyedai tokea edeni kuwa hakika hamtakufa, maana unapomwambia mfu "tutakukumbuka daima" inamana unaamini anakusikia huyu mfu kwahiyo iwe ni kama faraja kwake maana atakumbukwa daima. 

2. Inakuwa inaonyesha kuungana na shetani mkono kuamini kuwa Mungu ni mwongo aliposema kuwa "Baada ya kifo hukumu(mhuri).WAEBRANIA 9:27 na hivo hili neno R.I.P. yaani PUNZIKA KWA AMANI linakua n kama ombi au wakati mwingine kama amri kwa Mungu  kwamba hata kama mtu kafia uovuni basi  hukumu ya Mungu ibadilike na kuwa kinyume na huyu mfia uovuni apunzike kwa amani(tumaini) ambapo hili halipo wala halitawahi kutokea "Kwa kuwa mimi BWANA MUNGU sinakigeugeu.....MALAKI3:6"

 3. Kuendeleza udanganyifu na kufarijiana kuwa hata mtu afie dhambini anakuwa amepunzika kwa amani yaani matumaini.   Neno la Mungu linapinga vikali hii dhana na badala yake Neno linasema wale tu wanaokufa wakiwa upande wa Bwana ndio wanaolala kwa punziko la amani yaani matumaini ya kumngoja Yesu kwa ajili ya wokovu,  maana Biblia inasema "......Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam asema Roho, wapate KUPUNZIKA BAADA YA TAABU ZAO, KWA KUWA MATENDO YAO YAFUATANA NAO. Ufunuo14:13"

4. Kumrahisishia shetani kupandikiza imani ya UMIZIMU   mawazoni mwa watu wanaopenda kutumia maneno hayo ya R.I.P. na mengineyo yanayofanana na hayo, maana hili huathiri na kurithishwa hadi vizazi vijavyo kuamini kuwa wafu wapo mahali fulani na bado wanaishi na hivo tunaweza kuwaomba au kuwaombea chochote na kikawa, soma "1Samweli28:3-25"

         HITIMISHO
📩Neno la Mungu lipo wazi na lina mafungu mengi sana yanayoonyesha hali halisi kuwa mwanadamu aliumbwa kwa udongo na akifa anarudi udongoni hadi siku YESU  atakaporudi kutwaa walio wake na kutoa hukumu kwa shetani na wote walio upande wake maana baada ya dhambi Mungu alisema ".....Kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi. MWANZO 3:19" kwahiyo wafu wote wapo mavumbini wamelala. 

📩 Nawasihi wapendwa turekebishe mienendo yetu tungali hai maana hakuna lolote wala wala chochote wala yeyote atakayefanya tufutiwe makosa au dhambi au wema wa upande tuliofia.  Yaani kama ni dhambini itabaki hivohivo hadi siku ya mwisho hata kama uombewe vipi huo ni udanganyifu wa shetani haibadili chochote kukingana na Neno la Mungu,,,,,, na pia kama utafia  kwa Yesu itabaki hivohivo hadi siku ya mwisho.

📩 MUNGU ATUSAIDIE SANA NA KUTUSHINDIA MAANA SHETANI ANA NJIA NYINGI SANA ZA KUTUANGUSHA NA KUJIKUTA TUPO UPANDE WAKE PENGINE PASIPOKUJUA.

 
MUNGU ATUTIE NURU NA NGUVU ZAIDI, BARIKIWA

Je una taarifa ya kusisimua kuhusu dini unataka tuchapishe,tafadhali tuma kupitia whatspp +255759701713

No comments