kuchagua mwenza ktk ndoa
KABLA YA KUINGIA KWENYE NDOA, TAMBUA HISTORIA YA KIAFYA YA MCHUMBA WAKO.
Baada ya uumbaji wa Mungu kila kilichoumbwa na Mungu kilikuwa chema, magonjwa na Mambo mengine ambayo yanatupa changamoto katika Maisha yetu ni matokea ya Uovu wa mwanadamu wa kwanza yaani Adamu na Hawa.
Ndoa ni mkataba wa kudumu ambao haupaswi kuvunjwa na Mtu awaye yoyote maana Mungu wetu huchukia suala la Wana Ndoa kuachana.
Malaki 2:16
"Maana mimi nakuchukia KUACHANA, asema BWANA, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana."
Kwa sababu Mungu wetu wa Mbinguni huchukia anaposhuhudia Wana Ndoa wakiachana, ni Muhimu suala la afya pia kulitazama kikamilifu ili baadae lisiwe kikwazo mpaka kuchochea ugomvi ndani ya Ndoa.
Sisemi kwamba Usiolewe/kuoa mwenye matatizo ya kiafya, baali nakushauri ujue vyema Hali ya kiafya ili unapofanya maamzi uambatane nae ukiwa ni mwenye taarifa sahihi juu ya magonjwa/Ugonjwa unao msumbua mchumba wako.
Yupo ambae ana tatizo la Kifafa, Matatizo ya kiukoo, Kukojoa akiwa usingizini N.K
Kuwa na taarifa mapema itakufanya kujiandaa vyema kisaikolojia namna ya kuishi nae, kuliko kukutana na miongoni mwa magonjwa ndani ya Ndoa. Hii inaweza kuchochea msongo wa mawazo.
Lakini pia wewe ambae unayechumbia/Kuchumbiwa ni Muhimu Kama unalo tatizo la kiafya useme mapema ili kukufanya uishi maisha ambayo hutalaumiwa kila siku.
Kuficha taarifa sahihi za kiafya ni kuandaa bomu ambalo litaisambaratisha ndoa yako, maana mwenzi wako akigundua hatakuwa na Imani na wewe, na Hali hiyo ikitokea katika ndoa tayari ndoa hiyo imeelekea Mochwari.
Amua Leo kuwa muwazi kwa mchumba wako ili usije kuingia katika ndoa na Bomu la kuwasambaratisha.
ASANTE.
The Light Of Universe Ministry
Mwl Ejide Andrew Noah
+255743154575.
Post a Comment