Hongo ya Ngono!
ITAKUWA NI KILIO NA UCHUNGU SIKU UKIJUA NIA YA UNAYE MVULIA NGUO ZA NDANI KILA MARA.
Siku moja nilikuwa nikiwasiliana na rafiki yangu(Binti), nikabanwa kiasi sikuweza kuwasiliana nae Kama mwanzo maana kazi zilinifanya niwe bize sana.
Siku moja nikamtafuta ili kumjulia hali yake, ndipo akanieleza haya maneno;
"Yaani Kama tungekuwa tupo katika mahusiano na ukawa umeshafanya mapenzi na mimi, Mara gafla ukawa kimya kiasi hicho, ningeliumia Sana na ningekuchukia na wanaume wote maana ningekuona wewe ulikuwa na lengo la kunichezea tu". Mwisho wa kunukuu
Maneno Yale yalinifanya nitafakari sana na kujiuliza maswali ambayo kiasi kwamba ikanichukua muda, na hatimae nikapata Elimu tosha juu ya kauli yake.
Idadi ya watu wengi wanapoanzisha mahusiano, hukimbilia katika kufanya mapenzi(Uasherati) ili iwe Kama kiashiria kuwa wanapendana, kumbe sio.
Mara ya kufanya tendo hilo wapo wengi huwa wanaachwa siku hiyo hiyo maana kila aanzishae Jambo huwa ana kusudi lililofichika ndani yake.
Katika Eneo hili asilimia kubwa wanaoumia zaidi ni mabinti(Wanawake), maana wengine hutoa penzi Kama zawadi kwa Mpendwa wake akiamini anatia sukari katika Chai ili inyweke bila shida.
Watu wengi mioyo yao imejawa na vilio, machungu yasio na majibu kwa sababu walikubali kuvua nguo zao ili kudumisha penzi lao na mwisho wa siku wameachwa njia panda.
Kwako Dada, Tambua thamani yako kuwa ipo katika mwili wako, ukiruhusu kila mwanaume aufinyange atakavyo ni dhahiri utakuwa kiwanja Cha mazoezi ya watu kuelekea katika kiwanja Cha mashindano ya kudumu milele.
Tabia ya kupenda kumvulia mwanaume nguo zako za Ndani haiwezi kuchochea upendo wa Kweli zaidi tu utakuwa unatoa hongo ya ngono ili upendwe, lakini matokeo yake ni Mabaya kuliko uwazavyo.
Mungu amemuumba mtu Mwanaume na mtu mwanamke, hivyo unapaswa ujitunze kwa ajili ya Mumeo na sio vibaka wa mtaani.
Epukana na vilio vya kuumizwa katika mahusiano kwa kumkiri Yesu Kristo kuwa ni BWANA na Mwokozi wako ili akupe macho ya rohoni umjue aliye wako.
Kubali kuongozwa na Roho Mtakatifu, kamwe hutojuta kuongozwa nae maana yeye atakuonyesha njia yenye furaha, Upendo na utulivu.
ASANTE.
The Light Of Universe Ministry
Mwl Ejide Andrew Noah
+255743154575.
Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv
Post a Comment