amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Ijumaa 07/08/2020
*MUNGU HUTOA RASILIMALI*
*Hata kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea, wakasema, … Uwaage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula. … Wapeni ninyi vyakula. Wakamwambia, Hamna kitu hapa ila mikate mitano na samaki wawili. Akasema, Nileteeni hapa. akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano .... Wakayaokota masazo ya vipande vya mikate, vikapu kumi na viwili, vimejaa.* Mathayo 14:15-20
📝 Somo la kina la kiroho kwa wafanyakazi wa Mungu limefungwa ndani ya mfano huu.... Katika kumtegemea Mungu kabisa, Yesu alichukua akiba ndogo ya mikate; na ingawa palikuwa na chakula kidogo tu kwa familia yake ya wanafunzi, hakuwaalika kula, bali alianza kuwagawia, akiwaambia wawahudumie watu.
📝 Chakula kiliongezeka mikononi mwake; na mikono ya wanafunzi, iliponyoshwa kwa Kristo, Yeye mwenyewe akiwa ni Mkate wa Uzima, kamwe haikuwa mitupu. Akiba ndogo ilitosheleza kwa wote. Baada ya mahitaji ya watu kukidhiwa, vipande vilikusanywa, na Kristo na wanafunzi wake walikula chakula hicho cha thamani, kilichotolewa na Mbingu.
📝 Wanafunzi walikuwa ni mkondo wa mawasiliano kati ya Kristo na watu. Hii inapaswa kuwa faraja kubwa kwa wanafunzi wake leo. Kristo ni Kiini kikuu, Chanzo cha nguvu zote. Wanafunzi wake wanapaswa kupokea mahitaji yao kutoka Kwake... .Kadiri tunavyoendelea kutoa, tutaendelea kupokea; na kadiri tunavyozidi kutoa, ndivyo tunavyozidi kupokea...
📝 Zingatia dimbwi lile ambalo hupokea maji ya mbinguni lakini halina mlango wa kutolea. Si baraka kwa mtu yeyote, lakini kwa ubinafsi wa kutuama linatia sumu hewa inayolizunguka. Sasa angalia kijito kinachotiririka kutoka kando ya mlima, kikiburudisha ardhi yenye kiu ambayo hupita juu yake.
🔘 *Ni baraka iliyoje! Mtu angefikiri kwamba katika kutoa hivyo kwa ukarimu kingeliweza kumaliza akiba zake. Lakini sivyo. Ni sehemu ya mpango mkubwa wa Mungu kwamba kijito ambacho kinatoa kamwe hakitahitaji; na siku hadi siku mwaka kwa mwaka kinapita njiani, daima kikipokea na kutoa.*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv
Post a Comment