amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Ijumaa 28/08/2020

*BABA KWA MASKINI*

*Nalikuwa baba kwa mhitaji, Na daawa ya mtu nisiyemjua naliichunguza.*
Ayubu 29:16

🔰 Huu ulikuwa ni ushahidi kwamba Ayubu alikuwa na haki ambayo ilikuwa inafanana na aina ile ya Kristo. Kupitia kwa Yesu watu wanaweza kuwa na roho ya huruma kwa wahitaji na waliodhikishwa.... Alishuka kufikia aibu ya hali ya chini kabisa naye alikuwa mtiifu hadi kifo, kifo cha msalaba, ili apate kutuinua sisi kuwa warithi pamoja na Yeye. 

🔰 Ulimwengu wote ulikuwa na hitaji ya kile ambacho Kristo peke yake angeliweza kuwapa. Yeye hakujitenga na wale ambao walimwomba msaada. Hakufanya kama vile wengi wanavyofanya sasa, na kusema, Natamani wasingenisumbua na mambo yao. Mimi ninataka kuhidhi fedha zangu, kuiwekeza katika nyumba na ardhi. Yesu, Mkuu ya mbinguni, aligeuka kutoka kwa ufahari wa nyumba Yake ya mbinguni, na kwa kusudi la neema ya moyo wake alionesha tabia ya Mungu kwa wanadamu kote ulimwengu. 

🔰 Ondoa umaskini, nasi hatutakuwa na njia ya kuelewa rehema na upendo wa Mungu, hakutakuwa na njia ya kumjua Baba mwema wa mbinguni mwenye huruma. Kwanza tosheleza mahitaji ya maisha ya wahitaji na utulize mahitaji na mateso yao ya kimwili, nawe utapata njia ya wazi kwenda moyoni, ambapo utaweza kupanda mbegu njema za wema na dini. 

🔘 *Kamwe injili haileti sura ya kupendeza kuliko pale inapowafikia wale wahitaji na maskini kabisa.... Kweli kutoka katika Neno la Mungu unaingia ndani ya kibanda cha mkulima mdogo na kuangaza nyumba ndogo sahili za vijijini za maskini... .Miale kutoka kwa Jua la Haki huleta furaha kwa wagonjwa na watesekao. Malaika wa Mungu wako pale.... Wale ambao walikuwa wamechukiwa kabisa na kutelekezwa wanainuliwa kupitia imani na msamaha kufikia hadhi ya kuwa wana na binti za Mungu. Ukristo ni faraja ya maskini.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

Je una taarifa ya kusisimua kuhusu dini unataka tuchapishe,tafadhali tuma kupitia whatspp +255759701713

No comments