amka na Bwana

KESHA LA ASUBUHI

Alhamisi 06/08/2020

*MJAKAZI MDOGO AMSHUHUDIA MUNGU*

*Basi Naamani, jemadari wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa mbele ya bwana wake tena alikuwa mtu hodari wa vita; lakini alikuwa mwenye ukoma. Na Washami walikuwa wametoka vikosi, wakachukua mfungwa mmoja kijana mwanamke kutoka nchi ya Israeli; naye akamhudumia mkewe Naamani. Akamwambia bibi yake, Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake.* 2Wafalme 5:1-3

💎 Mtumwa, mbali na nyumbani kwake, hata hivyo, mjakazi huyu bado alikuwa mmoja wa mashahidi wa Mungu, akitimiza kusudi ambalo kwalo Mungu alikuwa ameichagua Israeli kama watu wake. 

💎 Alipokuwa akihudumu katika nyumba hiyo ya wapagani, huruma zake ziliamka kwa niaba ya bwana wake; naye, akikumbuka miujiza ya ajabu ya uponyaji iliyotendwa kupitia kwa Elisha, alimwambia bibi yake, "Laiti bwana wangu angekuwa pamoja na yule nabii aliyeko Samaria! Maana angemponya ukoma wake." Alijua kwamba nguvu za Mbingu zilikuwa pamoja na Elisha, na aliamini kuwa kupitia kwa nguvu hizi Naamani angeweza kuponywa. 

💎 Mwenendo wa mjakazi huyu mateka, jinsi ambavyo alienenda katika nyumba ile ya kipagani, ni ushahidi wenye nguvu wa nguvu ya mafunzo ya awali ya nyumbani. Hakuna dhamana ya juu zaidi ya ile iliyokabidhiwa kwa akina baba na akina mama kuhusu utunzaji na mafunzo ya watoto wao...

💎 Hatujui ni katika mwelekeo gani watoto wetu wanaweza kuitwa kuhudumu. Wanaweza kutumia maisha yao ndani ya mazingira ya nyumbani; wanaweza kujihusisha na kazi za kawaida katika maisha, au kwenda kama walimu wa injili katika nchi za kipagani; bali wote sawa wanaitwa kuwa wamisionari kwa Mungu, wahudumu wa rehema kwa ulimwengu.... 

🔘 *Wazazi wa huyo mjakazi Mwebrania, walipomfundisha juu ya Mungu, hawakujua majaliwa yake yangelikuwaje. Lakini walikuwa waaminifu kwa dhamana yao; na nyumbani kwa Mkuu wa jeshi la Shamu, mtoto wao alimshuhudia Mungu ambaye alikuwa amejifunza kumheshimu.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️

No comments