amka na Bwana

#KESHA_LA_ASUBUHI
JUMANNE, SEPTEMBA 1

SOMO: *KUTAKASWA KIKAMILIFU: MWILI, NAFSI NA ROHO*

*_💜Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili; bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo. 1 Wathesalonike 5:23_*

👉🏿Utakaso ulioelekezwa katika Maandiko Matakatifu unahusiana na mtu katika ukamilifu wake; roho, nafsi na mwili. Hapa ndipo lilipo wazo la kweli la kujitoa kikamilifu. Paulo analiombea kanisa la Wathesalonike waweze kunufaika na mbaraka huu. *_Mungu wa amani mwenyewe awatakase kabisa; nanyi nafsi zenu na roho zenu na miili yenu mhifadhiwe mwe kamili; bila lawama, wakati wa kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo 1Wathesalonike 5:23 ...._* 

 👉🏿Utakaso wa kweli ni kuendana kikamilifu na mapenzi ya Mungu. Mawazo na hisia za ukaidi vinadhibitiwa, na sauti ya Yesu huamsha maisha mapya, ambayo hujidhihirisha kikamilifu katika utendaji. Wale ambao wametakaswa kweli hawatafanya mitazamo yao kuwa ndio kipimo cha wema au uovu. Hawana ushupavu wa dini au kujihesabia haki; lakini wana wivu na nafsi, wakichelea nyakati zote, wasije wakashindwa kukidhi Vigezo vya ahadi waliyoachiwa .... 

👉🏿Utakaso wa Biblia haukujengwa katika msisimko mkali. Hapa ndipo wengi huelekezwa katika makosa. Wanafanya hisia zao kuwa ndio kigezo. Wanapojisikia kusisimka au kufurahi, hudai kwamba wametakaswa. Hisia za furaha au kukosa furaha sio ushahidi ya kwamba mtu huyo ametakaswa au la. Hakuna kitu kama utakaso wa papo hapo. 

 *👉🏿Utakaso wa kweli ni shughuli ya kila siku, inayoendelea maisha yote. Wale ambao wanapambana na majaribu ya kila siku, kushinda mielekeo yao ya dhambi, na kutafuta utakaso wa moyo na maisha hawajisifu kuwa ni watakatifu. Wana njaa na kiu kwa ajili ya haki. Dhambi huonekana kwao kuwa jambo ovu mno.*

*👉🏿 Utakaso wa kweli lazima ujumuishe kuifia nafsi na kufuata mapenzi ya Mungu kila siku.*

*_MUNGU ATUTAKASE NA KUTUBARIKI SOTE KWA NENO LAKE._*

No comments