amka na Bwana
KESHA LA ASUBUHI
Jumatatu 31/08/2020
*NINAWEZA KUNG'AA KAMA NYOTA MILELE NA MILELE*
*Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele.* Danieli 12:3
📜 Yeye ambaye amempangia "kila mtu kazi yake," kulingana na uwezo wake, kamwe hataruhusu utendaji wa kazi kwa uaminifu kupita bila kuzawadiwa. Kila tendo la uaminifu na imani litakamilishwa na ishara maalumu za fadhila na kibali cha Mungu. Kila mtendakazi amepewa ahadi: "Yeye aendaye na kulia, kuzaa mbegu ya thamani, bila shaka atakuja tena na shangwe, akileta maganda yake pamoja naye."
📜 Huduma yetu iwe fupi au duni kiasi gani, ikiwa kwa imani sahili tutamfuata Kristo, hatutasikitishwa na thawabu itakayopatikana. Thawabu ile ambayo hata aliye mkuu kabisa na mwenye hekima ya juu kabisa hawezi kuipata, mtu dhaifu kabisa na mnyenyekevu kabisa anaweza kuipokea. Lango la dhahabu la mbinguni hufunguliwa sio kwa wanaojiinua. Haiinuliwi kwa wenye kiburi rohoni. Lakini milango ya milele itafunguka wazi kwa mguso wa kutetemeka wa mtoto mdogo. Yatabarikiwa fidia ya neema kwa wale ambao wamefanya kazi kwa ajili ya Mungu kwa usahili wa imani na upendo.
📜 Nyuso za wale wanaofanya kazi hii zitavaa taji ya kujitoa kafara. Lakini watapata thawabu yao. Kwa kila mtendakazi wa Mungu wazo hili linapaswa kuwa kichocheo na kutia moyo. Katika maisha haya kazi yetu kwa Mungu mara nyingi inaonekana kama vile haizai matunda. Juhudi zetu za kufanya mema zinaweza kuwa za dhati na za kuvumilia, lakini bado tunaweza tusiruhusiwe kushuhudia matokeo yake. Kwetu juhudi hizi zinaweza kuonekana kama vile zimepotea. Lakini Mwokozi anatuhakikishia kwamba kazi yetu inakumbukwa mbinguni, na kwamba malipo hayawezi kukosekana.
🔘 *Ingawa maisha yake yanaweza kuwa magumu na ya kujikana nafsi, …machoni pa mbingu yatakuwa ni mafanikio, na atapewa nafasi kama mmoja wa watu wa Mungu walio katika daraja la juu. "Na walio na hekima watang'aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang'aa kama nyota milele na milele."*
*TAFAKARI NJEMA SANA*👮♂️
Je Una taarifa ya kusisimua kuhusu dini unataka tuchapishe,tafadhali tuma kupitia whatspp +255759701713
Post a Comment