amka na Bwana
#KESHA_LA_ASUBUHI
JUMATANO, AGOSTI 26
SOMO: *WAPATIE AHUENI WANAOKANDAMIZWA*
*_Jifunzeni kutenda mema; takeni hukumu na haki; wasaidieni walioonewa; mpatieni yatima haki yake; mteteeni mjane. Isaya 1:17_*
✝️Yesu, Mwokozi wa thamani kubwa, mtu wa mfano, alikuwa thabiti kama mwamba mahali ambapo ukweli na wajibu vilihusika. Na maisha yake yalikuwa mfano halisi wa uungwana wa kweli. Wema na upole vilitoa harufu nzuri kwa tabia Yake. Daima alikuwa na sura ya wema na neno la faraja na maliwazo kwa mhitaji na aliyeonewa...
👥Unapokutana na wale wenye dhiki na walioonewa, ambao hawajui ni njia gani ya kugeukia ili kupata nafuu, wekeni mioyo yenu katika kazi ya kuwasaidia. Sio kusudi la Mungu kwamba watoto wake wajifungie wenyewe kwa wenyewe, bila kujali ustawi wa wale wasio na bahati nzuri kama wao wenyewe. Kumbuka kwamba ni kwa ajili yao kama vile ilivyo kwa ajili yako Kristo amekufa. Upatanisho na fadhili zitaifungua njia kwa ajili yako kuweza kuwasaidia, kukufanya upate imani yao kwako, kuwatia moyo kuwa na tumaini na ujasiri.
👉🏿Hebu watu wasiruhusu mapatano yao ya shughuli za biashara kuondoa ubinadamu wao.... Maneno ya fadhili, mwonekano wa kupendeza, mwenendo wa kujishusha, ni vya thamani kubwa. Kuna uzuri katika maingiliano ya watu walio waungwana wa kweli.... Ni jinsi gani unarejesha na kuinua mvuto wa mapatano kama hayo kwa watu ambao ni maskini na wenye huzuni, walioshindwa na kuwekwa chini na magonjwa na umaskini! Je! Tuwazuilie zeri ile ambayo shughuli kama hiyo inaleta?
🙏🏾Kila tendo la haki, huruma, na ukarimu hufanya wimbo mbinguni. Baba kutoka katika kiti chake cha enzi huwaona wale wanaofanya matendo haya ya rehema, na kuwahesabu pamoja na hazina zake za thamani kabisa. Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa.
🙏🏾Kila tendo la huruma kwa wahitaji, watesekao, linachukuliwa kana kwamba limetendwa kwa Yesu. Unapowasaidia maskini, unapowahurumia watu wanaoteseka na walioonewa, na kuwa rafiki wa yatima, unajiweka wewe mwenyewe katika uhusiano wa karibu zaidi na Yesu.
*MUNGU AWABARIKI NYOTE.*🙏🏾👥
Je una taarifa ya kusisimua kuhusu dini unataka tuchapishe,tafadhali tuma kupitia whatspp +255759701713
Post a Comment