amka na Bwana

#KESHA_LA_ASUBUHI

JUMANNE, AGOSTI 25

SOMO: *WAVIKE NGUO WALIO UCHI*

*_Nalikuwa uchi, mkanivika. Mathayo 25:35, 36_*

✝️Kristo anasema, Ni mimi ndiye nilikuwa na njaa na kiu. Ni mimi ndiye nilikuwa mgeni. Ni mimi ndiye nilikuwa mgonjwa. Ni mimi ndiye nilikuwa gerezani.... Wakati wewe ulipojaza kabati lako la nguo kwa mavazi ya gharama, nilikuwa maskini. Wakati ulipofukuzia anasa zako, nilinyong'onyea gerezani. 

 👥Ulipokuwa unagawa posho ndogo ndogo za mkate kwa maskini wenye njaa, ulipotoa zile nguo laini ili kuwalinda kutokana na baridi kali ya theluji nyembamba, je! ulikumbuka kuwa ulikuwa unampa Bwana wa utukufu? Siku zote za maisha yako nilikuwa karibu nawe katika nafsi za hawa walioteseka, lakini hukunitafuta. Hutaingia katika ushirika pamoja na Mimi. 

 👥Katika ulimwengu wa wanaodai kuwa Wakristo kuna kiasi kikubwa kinachotumika kwa ubadhirifu wa kujionesha, kwa ajili ya vito na mapambo, ambacho kingelitosha kukimu mahitaji ya wote wenye njaa na kuwavika walio uchi katika miji na majiji yetu; lakini bado hawa wanaokiri kuwa wafuasi wa Yesu aliye mpole na mnyenyekevu hawahitajiki kujinyima chakula bora au mavazi ya kuridhisha. 

 👥Je! Washiriki hawa wa kanisa watasema nini watakapokabiliwa katika siku ile ya Mungu na maskini, aliyeteseka, mjane, na yatima, anayestahili ambaye amepitia dhiki kali kwa ajili ya mahitaji madogo madogo ya maisha, huku hawa wanaodai kuwa wafuasi wa Kristo walitumia fedha ambazo zingelitosha kukidhi mahitaji yao, kwa ajili ya mavazi ya gharama ya juu kupita kiasi, na mapambo yasiyo ya lazima ambayo yamekatazwa waziwazi katika Neno la Mungu? 

 👥Katika sura ya hamsini na nane ya Isaya kazi ambayo watu wa Mungu wanapaswa kuifanya katika shughuli za Kristo imewekwa wazi. Wanapaswa kuvunja kila nira, wanapaswa kuwalisha wenye njaa, kuwavika walio uchi.... Ikiwa watatekeleza kanuni za sheria ya Mungu kwa matendo ya fadhili na upendo, watawakilisha tabia ya Mungu kwa ulimwengu, nao watapata baraka tele za Mbingu.

*_TAFAKARI NJEMA EWE MWANA NA BINTI WA MFALMA💂🏽‍♀️👮🏼‍♀️

Je una taarifa ya kusisimua kuhusu dini unataka tuchapishe ,tafadhali tuma kupitia whatspp +255759701713

No comments