Tai ktk dhoruba
Tai wa safu za milima mirefu wakati fulani husukumwa na dhoruba hadi bonde jembamba la milima. Mawingu mazito humfungia ndani ndege huyu mkuu wa msituni, giza lake humtenga na vimo vyenye mwanga wa jua alipotengeneza nyumba yake.
Nguvu zake za kujiokoa huwa zisizo na matunda.
Huruka huku na huku, akipiga hewa kwa mbawa zake zenye nguvu na kuamsha miangwi ya mlima kwa kilio chake.
Baada ya muda mrefu, kwa sauti ya ushindi, anaruka juu na kuyapenya mawingu na kuwa tena katika mwanga mpevu akiviacha giza na dhoruba chini kabisa.
Hivyo twaweza kuzungukwa na matatizo, kukata tamaa na giza.
Uongo, misiba, dhuluma, vimetufungia ndani.
Kuna mawingu ambayo hatuwezi kuyaondoa.
Tunapigana na mazingira bila mafanikio.
Kuna njia moja, na moja pekee ya kujiokoa.
Mbali zaidi na mawingu kuna mwangaza wa nuru ya Mungu.
Twaweza kuinuka kwa mbawa za imani katika mwangaza wa jua la uwepo wake.
Happy Sabbath day!
Post a Comment