Mungu pekee ndio msaada

Kuna mambo Mungu anakuruhusu Uyapitie ili uje kuwa msaada kwa wengine hapo baadae. 

Masomo ya namna hii wakati mwingine yanaambatana na maumivu, kukataliwa na aibu ila ndio sehemu ya mtaala wa somo lako ili uandaliwe vizuri. 

Unapitia makosa ambayo ulidhani usingeweza kuyafanya ili ukikutana na mtu aliyekosea USIMHUKUMU. 

Unapitia maumivu yanayodhihirisha udhaifu wako, ili ukikutana na mtu aliyepatwa na aibu UMSITIRI. 

Unakutana na kufeli katika kitu ulichokuwa na uhakika 100% kuwa utafaulu ili ukikutana na aliyefeli usimuone mzembe bali UMTIE MOYO. 

Unapitia hali ngumu ya maisha na kukosa pesa, ili siku mtu akihitaji msaada wako unakuwa unaelewa maumivu ya kushinda njaa na kutokuwa na pesa. 

Unapitia kipindi unabaki peke yako na hakuna wa kukusaidia ili siku ukikutana na mtu aliyeachwa na awapendao uelewe maumivu anayopitia na UMSAIDIE. 

Nakuombea, Mungu akupe nguvu usikimbie darasa bali UFAULU.

By Ev.Dalali David

Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv

Barikiwa

No comments