msamaria mwema! Tujifunze

Habar ya asubuh wapendwa binafs napenda Sana kumshukuru Mungu kwa kuiona siku nyingine tofauti na Jana.

Leo nilitamani tushirikishane kujifunza juu ya kisa Cha msamaria katika Luka 10;30 ambachoo naamini kabisaa sio kigeni masikioni mwetu.

Ktk kisa hiki tujifunze habar ya watu watatu wenye falsafa zao tofauti ambaoo kimsing ndioo nature ya watu tulionao kanisani leo.

1; Ni wanyang'anyi wenye falsafa isemayo,, CHAKO NI CHANGU NA NITAKICHUKUA!
Hawa hafananishwa na watu ambao wanashindwa kutambuaa kuwa Mali na  vyote viijazavyo ni Mali ya Bwana hivyo wanapopata hiyo Mali au mafanikio Fulani wanaamini ni kwa nguvu zao na Mara nyingi hawana shukrani kwani waamini ilikuwa ni stahili yao kupata walichokipata na s vinginevyo. Je ni Mara ngapi umemshukuru Mungu kwa kilee kidogo anachokupatia?? Au unadhani no stahili yako kuwa nacho??

2; Ni makuhani wenye falsafa isemayo,, CHANGU NI CHANGU NA NITAKITUNZA.
Makuhani baada ya kuniona aliyepigwa walipigwa wakapita kando ya njia,, Hawa hufananishwa na wale ambao wanakarama ya utumishi aidha kuimba au kuhubir au pengine wanauwezo kifedha ambao unaweza kusogeza kazi ya Mungu lakini ni wabinafsi wanang'ang'ania walivyonavyo na hawataki kujitoa kwaajili ya kusongeza kazi ya Bwana kwa namna moja nyingine! Je ni Mara ngapi nimekuwa mbinafsi na kushindwa kujitoa kiutumishi ilihali ninajua ninakarama?? Je ni Mara ngapi nimeiwezesha kazi ya Mungu kusongaa mbele kwa kilee kidogo nilichokuwa machoo??
    Ombi langu asubuh hii ya leo, Mungu anisaidie niache ubinafsi na ninatamani lingekuwa ombi lako piaa pamojaa nami

3; Ni msamaria mwenye falsafa isemayo,, CHANGU NI CHAKO NA TUTASHARE.
Hii ndioo Tabia ya Mkristo wa kweli, msamaria alijitoa kikamilifu kumsaidia mtu asiyemjua lkn hii yote ni kwasababu alikuwa na utu na huruma pia!! Yesu alipowana wahitaji aliwahurumia akawasaidia! Je ni Mara ngapi tunawaona watu kma Yesu alivyona ,,Je Ni Mara ngapi tumejitoa kuwasaidia wale wanaohitaji msaada wetu japo kwa uchache hata kma hatuwafahamu??
   Tunapaswa kuiga tabia ya msamaria na ya Yesu ya kuwahurumia watu na kuwasaidia pale tunapowezaa!! 

Mungu abariki tafakar hii ktk jina lakee Amina!

Muwe na siku njemaa!🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏🙏

No comments