mavazi na Ukristo
Tabia ya mtu hutambuliwa kutokana na mtindo wa mavazi yake.
Muonjo wa kiungwana, akili iliyojengwa, vitadhihirishwa katika uchaguzi wa mavazi mazuri sahili. Unyofu na usahili wa nguo vikiunganika na mwenendo mzuri, vitaenda mbali katika kumzingira kijana mwanamke kwa hali ya kujitunza kwa utakatifu itakayokuwa ngao kwa mitego maelfu.
Hebu wasichana na wavulana wafundishwe kwamba ustadi wa kuvaa vyema huhusisha uwezo wa kuchagua mavazi ya heshima na yenye kuwasitiri.
Ni vema kupenda uzuri na kuutamani; ila Mungu anatamani tupende na kutafuta uzuri wa juu ule usioharibika.
Uchaguzi bora zaidi katika uzalishaji wa uwezo wa kibinadamu hauna uzuri uwezao kulinganishwa na uzuri wa tabia ambao machoni pa Mungu ni wa "gharama ya juu."
Hivyo, katika mavazi kama ilivyo kwa vitu vingine pia ni nafasi yetu kumtukuza Muumbaji wetu.
Anataka nguo zetu ziwe maridadi na zinazokubaliana na afya, lakini pia ziwe za stara.
MUNGU ATUSAIDIE SANA.
Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv
Post a Comment