maadui 3 wa imani yetu ktk Kristo
*MAADUI WATATU WA IMANI YETU UNAOPASWA KUWASHINDA ILI UMPENDEZE MUNGU*
Wapo maadui watatu wanaopambana na mtu aliyeamini ili asimpendeze Mungu.
*➡Maadui hawa watatu usipowashinda hauwezi kumpendeza Mungu kamwe na wala hauwezi kutembea na mibaraka ya Mungu maishani mwako*
Maana imeandikwa hivi
*👉Ufunuo 2:7 Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.*
Kwahiyo ili ule matunda ya mti wa uzima, sharti ni moja 👉USHINDE.
Sasa twende kuwaona maadui watatu wa imani unaopaswa kuwashinda kila iitwapo leo ili uishi katika mapenzi ya Mungu na utembee na mibaraka yako.
*1.MWILI*
Adui wa kwanza unayetakiwa kumshinda ni mwili.
Biblia inasema hivi
*👉1 Wathesalonike 4:4 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima;*
Biblia inamtaka kila mtu aliyemuamini Yesu AJUE KUUWEZA MWILI WAKE.
➡Kwa maana nyingine ni kuwa *MWILI HAUPASWI KUKUENDESHA WEWE, ISIPOKUWA WEWE NDIYE UNAYEPASWA KUUNDESHA MWILI WAKO*
Ukikubari kuendeshwa na mwili uwe na uhakika hauwezi kuyafanya mapenzi ya Mungu.
➡UKITAWALIWA NA MWILI UTATENDA UOVU TU.
Maana imeandikwa hivi.
*◾Wagalatia 5:19-21*
*19 Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,*
*20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,*
*21 husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.*
Kwahiyo mwili ni adui yako wa kwanza unayepaswa kumshinda ili Umpendeze Mungu.
*◾JINSI YA KUUSHINDA MWILI*
1.Tafuta kuenenda kwa msaada wa nguvu za Roho mtakatifu
Biblia inasema.
*👉Wagalatia 5:16 Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.*
Ukienenda kwa msaada wa nguvu za Roho mtakatifu matokeo yake itakuwa.
*I.Utamzalia Mungu matunda mema*
Maana biblia inasema hivi
*◾Wagalatia 5:22-23*
*22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,*
*23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.*
II. Mwili wako utakuwa hekalu la Roho mtakatifu.
*👉1 Kor 6:19 Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;*
Faida ya kuwa hekalu la Roho mtakatifu
*➡Unakuwa Mali ya Mungu inayolindwa mchana na usiku dhidi ya mwovu shetani*
KWAHIYO TAFUTA KUJAZWA NGUVU ZA ROHO MTAKATIFU ILI UUSHINDE MWILI
Jambo lingine la kufanya ili uushinde mwili ni hili lifuatalo.
*2.KUFUNGA NA KUOMBA*
Mtu asiye na mda wa kufunga na kuomba ni rahisi sana kuanguka katika vishawishi mbalimbali vya mwili.
Maana imeandikwa
*👉Mathayo 26:41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.*
Ili usiingie katika majaribu ya mwili shariti ni moja tu uombe, usipoomba mwili utakuendesha tu.
*◾Kijana asiyefunga na kuomba ni rahisi kuanguka kwenye tamaa za Mwili*
*◾Mchungaji asiye na mda wa kufunga na kuomba ni rahisi kujaribiwa na mwili wake na kujikuta anafanya mambo ya aibu*
➡Nasema hivi mtu yeyote asiyefunga na kuomba ni ngumu kuzishinda tamaa za mwili kwahiyo ili uushinde mwili jifunze kufunga na kuomba.
*3.Usikae mahali penye vitu vinavyoamsha tamaa za Mwili*
Ili uushinde mwili jifunze pia kujitenga na maeneo yote yanayoweza kuuamsha mwili.
Imeandikwa hivi
*👉Wimbo ulio bora 8:4 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwani kuyachochea mapenzi, au kuyaamsha, Hata yatakapoona vema?*
Ni hivi unaweza kuziamsha tamaa za mwili kutokana na mazingira uliyopo.
Hivyo ili uushinde mwili jifunze kujitenga na vitu vyenye ushawishi mbaya kama *👉kuangalia picha za ngono, mazungumzo mabaya, mafundisho yanayoshawishi ngono, kusikiliza nyimbo za kidunia, kuvaa nguo za kikahaba n.k* kwa kufanya hivi unaweza kuushinda mwili.
*4.Kuliweka neno moyoni mwako*
Jambo lingne linaloweza kukufanya uushinde mwili ni kuliweka neno moyoni mwako.
Biblia inasema hivi
*👉ZABURI 119:11 Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.*
Pia imeandikwa
*👉ZABURI 119:105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.*
Kwahiyo ili uushinde mwili na tamaa zake hakikisha ndani yako Kuna upanga wa roho ambao ni neno la Kristo.
*➡Ukiushinda mwili ni rahisi kumpendeza Mungu na ni rahisi kutembea na mibaraka ya Mungu*
MWISHO
*👉 2 Timotheo 2:22 Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.*
Kwa Leo niishie hapa tutaendelea na ujumbe huu kipindi kijacho.
Mungu awabariki sana🙏
WhatsApp 0657117595
Mwl.Joseph Leonard
Usisahau ku subscribe YouTube channel yetu ya BinagoTv
Safi sana, nimependa umekuwa mfano mzuri, hujafuta mwandishi wa ujumbe, Mungu wa mbinguni akubariki sana 🙏
ReplyDelete