Kuwekwa Huru

SOMO: KUFUNGULIWA KUTOKA VIFUNGO VYA GIZA

📖  Luka 4:18-19

18 Roho wa Bwana yu juu yangu, 
Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. 
Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, 
Na vipofu kupata kuona tena, 
Kuwaacha huru waliosetwa,

19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.

➡️Watu wengi, waliokoka na wasiookoka wapo katika hali hii ya vifungo kwa kujua ama kwa kutojua, hivyo naamini baada ya somo hili tutapata ufahamu mdogo juu ya nini tufanye katika kuepuka vifungo hivi. 

👉🏾Kabla ya kufika hatua ya kufunguliwa kutoka kwenye vifungo vya giza ambapo hasa ni msingi wa somo letu, tutaangalia maana ya maneno yatakayotumia kwenye somo hili.

👉🏾Tutaangalia historia ya vifungo vya kimwili katika agano la kale na agano jipya (katika mfano wa kiroho na kimwili)

👉🏿 Pia tutaangalia sababu ya vilizowapeleka watu vifungoni utumwani (agano la kale) na sababu zinazotupelekea vifungoni (utumwani) katika maisha yetu. 

👉🏾Tutaangalia namna ambavyo shetani anavyowafunga watu (mbinu za shetani).

👉🏾Tutaingia sasa kwenye somo letu namna ambavyo tunaweza KUFUNGULIWA KUTOKA VIFUNGO VYA GIZA

👉🏿 Leo tunaendelea na somo letu katika kipengele cha pili:-

SABABU KUPELEKEA KWENDA KIFUNGONI (UTUMWANI)

👉🏿 Hila na chuki – Yusufu anapelekwa utumwani kwa Potifa kwasababu ya hila na chuki za ndugu zake. Mwanzo 37:18-36

👉🏿 Uasi – Taifa la Israeli lilikua likijikuta likipigwa na adui wakati mwingine kupelekwa utumwani kwasababu ya kumuasi Mungu. Yeremia 34:17, 2Wafalme 15:27, 23:36-37.

👉🏾Kutosikiliza na kutii sauti ya Mungu kupitia watumishi wake. 2 Wafalme 18:11,12, 

 Yeremia 18:10

ikiwa watatenda maovu mbele za macho yangu, wasiitii sauti yangu, basi nitaghairi, nisitende mema yale niliyoazimia kuwatendea.

Kumbe taifa la Israel lilijikuta kwenye kifungo kwasababu ya kutosikia na kutii sauti ya Bwana. 

👉🏾Utumwa wa wazazi wao. Kutoka 21:4-5. Lakini pia kuna watu walijikuta watumwa kwasababu ya kuzaliwa na wazazi waliopo utumwani. 

👉🏿 Maamuzi au matakwa(hiyari) ya mtu mwenyewe baada ya kuishiwa au kuchoka kusubiri, kutafuta mbadala wa kukabiliana na hali aliyonayo au anayopitia. Luka 15:14-15. Mwana mpotevu anaingia katika kifungo kwahiayari yake baada ya kuchezea urithi wake kwa anasa, njia pekee au chaguo pekee alilokuwa nalo ni kujipelekwa utumwani ili aweze kuishi.

➡️Tukutane wiki ijayo kwa muendelezo wa somo hili, mpendwa nakusihi sana jitahidi sana kulisoma kuna mambo mengi sana ya kujifunza humo.

➡️Mungu akubariki sana sana. 
➡️Unaweza ukashare ujumbe huu ili uwafukie wengi na usisahau kulike ukurasa huu kwaajili ya mafundisho.

📌Pia katika ukurasa huu unaweza kuuliza maswali yoyote ya Biblia yanayokutatiza yanayohitaji majibu, lakini unaweza pia kutuma mahitaji kwa ajili ya maombi na maombezi. 

🔗Usisahau kubonyeza hapa halafu bonyeza LIKE ili uendelee kuwa nasi-https://www.facebook.com/Adonaielohi

Niliyekuletea somo hili ni mtumishi:-

 Elisha Samson Bungwa
☎+255716472317🥏
☎+255629083835
☎+255747223748 
📧 samsonelishajr@gmail.com 

THE FREE PENTECOSTAL CHURCH OF TANZANIA (FPCT)
EWC KIJICHI

Dar es Salaam

         SHALOM SHALOM ✋

No comments