Facebook yafuta ujumbe wa Gwajima kuhusu Corona na 5G
Kampuni ya Facebook inayomiliki mtandao wa Instagram imeufuta ujumbe wa video uliokuwa umepakiwa na mhubiri Mtanzania Josephat Gwajima kuhusu virusi vya corona.
Kwenye ujumbe huo kwenye Instagram na IGTV, askofu Gwajima alikuwa amedai kwamba janga la virusi vya corona lina uhusiano na juhudi za kusambaza teknolojia ya kisasa ya mawasiliano ya 5G.
Alikuwa ameishauri Tanzania isiikumbatie teknolojia hiyo.
Facebook imesema ujumbe huo wa Gwajima umefutwa kwa kuwa unakiuka kanuni na masharti ya mtandaoni ya kampuni ya hiyo.
"Huwa tunazifuta taarifa za uzushi ambazo zimewaza kusababisha madhara moja kwa moja, ikiwa ni pamoja na ujumbe unaodai kwamba 5G inasababisha janga la virusi vya corona, na tunachunguza taarifa za aina hii," msemaji wa Facebook aliiambia BBC.
"Duniani, tumefuta mamia ya maelfu ya ujumbe wenye taarifa za uzushi kuhusu Covid-19 na tumekuwa tunawaelekeza zaidi ya watu 2 bilioni kwa habari na maelezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) na mamlaka nyingine za afya kupitia kituo chetu cha habari za Covid-19."
Post a Comment