amka na Bwana!
KESHA LA ASUBUHI
Ijumaa 17/07/2020
*NYUMBANI PAWE KIMBILIO KWA AJILI YA VIJANA.*
*Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu, anipokea mimi; na mtu akinipokea mimi, humpokea, si mimi, bali yeye aliyenituma.* Marko 9:37
📝 Nyumba zetu zinapaswa kuwa mahali pa kimbilio kwa vijana waliojaribiwa. Wengi wao wamesimama katika njia panda. Kila mvuto, kila wazo, huamua uchaguzi ambao unatengeneza majaliwa ya sasa na ya baadaye.
📝 Usijitenge mbali nao, bali sogea karibu nao. Walete katika sebule yako ya kuotea moto; wakaribishe kwenye madhabahu za familia yako. Kuna kazi ambayo maelfu wangepaswa kufanya kwa ajili yao. Kila mti katika bustani ya Shetani umening'iniziwa tunda la sumu lenye kushawishi, na ole imetamkwa juu ya kila mmoja anayelichuma na kulila.
📝 Uovu unawaita. Makimbilio yake yamefanywa angavu na ya kuvutia. Yana mapokezi kwa kila anayewasili. Kotekote kutuzunguka wapo vijana ambao hawana makazi na wengine wengi ambao nyumbani kwao hakuna nguvu za kuwasaidia, na kuwainua, na hivyo vijana hawa wanakwenda bila malengo wala mwelekeo katika uovu. Wanashuka katika uharibifu wakiwa karibu kabisa na milango yetu wenyewe.
📝 Vijana hawa wanahitaji mkono ulioonyoshwa kwao kwa huruma. Maneno ya fadhili yanayosemwa kwa usahili, kuzingatiwa japo kidogo tu, kutaondolea mbali mawingu ya majaribu yanayokusanyika juu ya roho. Onesho la kweli la huruma ya kimbingu lina nguvu ya kufungua mlango wa mioyo ambayo inahitaji harufu ya maneno kama ya Kristo na mguso sahili, laini wa roho ya upendo wa Kristo. Kama tungeonesha kuvutiwa na Vijana, kuwakaribisha nyumbani kwetu, na kuwazunguka kwa mivuto yenye kutia matumaini, yenye kusaidia, kuna wengi ambao kwa furaha wangeligeuza hatua zao kuelekea katika njia ya kwenda juu.
🔘 *Kumbuka kuwa furaha haitapatikana kwa kujifungia wenyewe kwa wenyewe, mkiridhika na kumimina upendo wenu wote kila mmoja na mwenzi wake. Tumia kila fursa ya kuchangia katika furaha ya wale walio karibu nawe.... Furaha ya kweli inaweza kupatikana tu katika huduma isiyo ya ubinafsi.*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮♂️
Post a Comment