Chaguo lako lipi???

Litakuwa jambo la huzuni siku ile ambapo watu watasimama wakikabiliana uso kwa uso na umilele.
Maisha yote yatajitokeza kama yalivyokuwa.
Anasa za dunia, Utajiri na heshima hazitaonekana tena kuwa ni za muhimu.
Watu wataona wazi kuwa ile haki waliyoidharau ndiyo pekee yenye maana.
Wataona kuwa walijenga tabia zao chini ya udanganyifu na mivuto ya shetani.
Vazi walilochagua ni kitambulisho cha ushirikiano wao na yule muasi mkuu.
Ndipo wataona matokeo ya uchaguzi wao.
Wataelewa kwamba uasi kwa amri za Mungu unamaanisha nini.
Hapatakuwa tena na wakati wa majaribio na rehema ili kujiandaa kwa umilele.
Ni katika maisha haya ndipo tunapaswa kujivika vazi la haki ya Kristo na kuzifanya tabia zetu kufaa kwa ajili ya makao ambayo Kristo ameyaandaa kwa ajili ya watakatifu.

Basi, jiangalieni mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafla,"
(Luka 21:34).

No comments