Amka na Bwana!


KESHA LA ASUBUHI

Sabato 23/05/2020

*DANIELI KIELELEZO CHA KIASI*

*Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Daniel, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya Mfalme. Na katika kila jambo la hekima na ufahamu alilowauliza mfalme, akawaona kuwa walifaa mara kumi zaidi ya waganga na wachawi waliokuwa katika ufalme wake.* Daniel 1:19,20.

💎 Mnamo miaka yao mitatu ya mafunzo, Daniel na marafiki zake walidumisha mazoea yao ya kiasi, na utii wao kwa Mungu, na utegemezi mkamilifu kwa uweza wake. Wakati ulipofika ambapo mfalme alitaka kutathmini uwezo wa ujuzi wao, walikaguliwa wao pamoja na vijana wengine, kwa ajili ya utumishi wa mfalme. Ufahamu wao wa kina,uchaguzi wao wa maneno na ubingwa wa lugha, vilidhihirisha hakika walikuwa bora katika nguvu na uwezo wa kiakili.

💎 Mungu daima huwaheshimu walio sahihi. Vijana wenye vipaji kutoka nchi mbalimbali zilizotekwa na Babeli walikusanywa pamoja, ila miongoni mwao hakuna waliowafikia kwa hekima na ujuzi vijana Waebrania.

💎 Mwonekano wa mauombo yaliyonyooka wenye nguvu, wakitembea kwa ukakamavu, nyuso zikijawa tabasamu, akili zikiwa angavu, wakipumua kwa uzuri---yote hayo yalidhihirisha heshima au mibaraka Mungu awapatiayo wale walio watiifu kwake.

💎 Licha ya vishawishi tele katika ikulu za anasa za Babeli vijana hawa walidumu kuwa waaminifu kwa Mungu. Vijana wa Leo wamezungukwa na vishawishi vya uovu na tamaa za anasa. Hasa katika miji mikubwa, kila kitu cha kushawishi uovu hufanywa rahisi na chenye mvuto. Wale ambao kama Danieli,wanakataa kujinajisi nafsi zao watavuna thawabu ya mazoea yao ya kiasi.

💎 Akili pevu ya Danieli na uthabiti wake na maamuzi, uwezo wake wa kujipatia maarifa na kupinga majaribu, vilitokana kwa kiasi kikubwa, na namna yake ya ulaji na mahusiano yake imara kwa Mungu.

🔘 *Simama imara katika utu uzima wako uliopewa na Mungu kama mwanamume na mwanamke. Mungu atakubariki uwe na mishipa mitulivu ya fahamu, ubongo unaochapa kazi, maamuzi sahihi na utambuzi makini. Vijana wa leo ambao huishi kwa kanuni pasipo kuyumba watabarikiwa kuwa na afya njema kimwili, kiakili, na kiroho.*

*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮‍♂️ 

No comments