Amka na Bwana!
KESHA LA ASUBUHI
Jumapili 17/05/2020
*FANYENI YOTE KWA UTUKUFU WA MUNGU*
*Basi mlapo au mnywapo, au mtendapo neno lolote fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.* 1Wakorintho 10:31
📜 Ili kuhifadhi afya, kuwa na kiasi katika mambo yote ni jambo muhimu -----kiasi katika kazi, kiasi katika kula na kunywa. Baba yetu wa mbinguni ametupatia nuru ya matengenezo ya afya ili wapendao usafi na utakatifu wajue namna ya kutumia kwa hadhari vitu vyema alivyowapatia,na kwa kujitawala nafsi katika maisha ya siku kwa siku wapate kutakaswa na ile kweli.
📜 Uangalifu mkuu ufanyike kuunda mazoea sahihi ya jinsi ya kula na kunywa. Chakula tunachokula kiwe kile ambacho kitatupatia damu nzuri. Viungo mbalimbali vya mwili vihusikavyo na usagaji wa chakula viheshimiwe. Mungu anatuhitaji, tuwe na kiasi katika mambo yote, tufanye yote tuwezayo kudumisha afya zetu. Uzoefu wetu wa kiroho hutegemea sana vile tulitendeavyo tumbo letu. Kula na kunywa kulingana na kanuni za afya hukuza utendaji mwadilifu.
📜 Kanuni sharti zitawale wala siyo tamaa au fahari. Ni jambo la thamani kuwa mkweli machoni pa Mungu. Anayo madai kwa wote wanaoshiriki huduma za kiroho shambani mwake. Anataka akili na miili yao itunzwe iwe katika uzuri wa hali ya juu kiafya, kila talanta na kipaji kiwe chini ya uongozi wa kimbingu, vikitenda kazi vyema na kwa usalama, kwa ufanisi wa juu kadiri mazoea yao ya kiasi yaruhusuvyo. Kiasi katika ulaji, kiasi katika unywaji, kiasi katika ulalaji,kiasi katika uvaaji ni moja ya kanuni kuu za maisha ya kidini. Ukweli upokelewapo kama kanuni iongozayo moyoni utautawala vyema mwili.
🔘 *Kadri unavyojali kutii kanuni za afya, ndivyo utakavyokuwa na uwezo zaidi wa kutambua majaribu na kumudu kuyapinga, na ndivyo utakavyomudu kugundua thamani ya mambo ya umilele. Hebu Mungu akuwezeshe kutumia vyema fursa na nafasi zijitokezazo kwako, ili siku kwa siku uweze kupata ushindi mpya, na mwisho upate kuingia mji wa Mungu, kama wale "walioshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo na neno la ushuhuda wao" Ufunuo 12:11)*
*MUNGU AKUBARIKI SANA*👮🏽

Post a Comment