Siku za mwisho ndio hizi! Au unataka uone dalili gani tena nyingine

#KAMA_ILIVYO_KUWA_WAKATI_WA_NUHU_NDIVYO_KUTAKAVYOKUWA_KUJA_KWAKE_MWANA_WA_ADAMU.

Luka 17:26 Na kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika siku zake Mwana wa Adamu.
27 Walikuwa wakila na kunywa, walikuwa wakioa na kuolewa, hata siku ile Nuhu aliyoingia katika safina, gharika ikashuka ikawaangamiza wote.

- Kati ya watu wengi wa dunia kabla ya gharika, ni watu wanane tu ndio waliamini na kutii Neno la Mungu kupitia kwa Nuhu.

Kabla Mtoa Sheria(Mungu) hajaja kuwaadhibu wasiotii, waasi wanaonywa ili watubu na kurudi katika utii; lakini kwa wengi maonyo haya yatakuwa ni bure.

Mtume Petro anasema," Katika siku za mwisho watakuja na dhihaka zao watu kwenye kudhihaki, wafuatao tamaa zao wenye, na kusema iko wapi ahadi ile ya kuja kwake?,  2 Petro 3:3,4.

Paulo anatuonya kwamba tutazamie maasi kuongezeka kadri mwisho unavyokaribia " Roho Anena wazi wazi, kwamba katika siku za mwisho baadhi watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani". 1 Timotheo 4:1.

 Mtume anasema kwamba " Katika siku za mwisho, kutakuwepo na nyakati za hatari". 2 Timotheo 3 :1. Na anaanza kutaja orodha ya dhambi zitakazooneka miongoni mwa walio na mfano wa utauwa.

Kadri muda wao wa rehema ulivyokaribia mwisho, watu wa kipindi cha Nuhu walijiingiza wenyewe  katika sherehe za kifahari.

 Wale waliokuwa na uwezo na mvuto walizifanya akili za watu zigeukie anasa, ili kwamba asije mmojawapo na ujumbe wa maonyo. Hatuoni hayo yakirudiwa katika siku zetu?

 Wakati watumishi wa Mungu wanatoa ujumbe kwamba mwisho wa kila kitu u karibu, ulimwengu unavutwa kwenye anasa.

Kuna  misisimiko ambayo inawafanya wawe tofauti na Mungu na kuwazuia watu wasiweze kuvutwa na ukweli  ambao ndio pekee utakaowaokoa Kutoka katika maangamizi yanayokuja.

Wakati watu mashuhuri walipojiridhisha kwamba isingewezekana ulimwengu kuharibiwa na maji , wakati ulipofika ulimwengu uliharibiwa  kwa maji.

Usichoke kuomba rehema kwa Mungu pia Liombee taifa letu Tanzania,Mungu Atuepushe na Corona!

No comments