Masanja na Covid-19 matatani kuwekwa ndani
MKUU wa Wilaya ya Mji wa Dodoma Patrobas Katambi amemtaka Msanii wa vichekesho nchini Emmanuel Mgaya maarufu kwa jina la Masanja mkandamizaji kuripoti Polisi ndani ya siku tatu baada ya kuonyesja mzaha katika ugonjwa wa virusi vya Corona.
Masanja alitupia video katika mitandao ya kijamii akifanya mzaha kwa kuhoji watu kuhusiana na ugonjwa wa Corona jana, ambapo baadhi ya watu aliokuwa akiwahoji, walisema wanahitaji covid-19 wapatiwe nyingi.
Alisema Masanja alifanya tukio hilo akitumia neno la kingereza la Covid-19, ambapo alitaka kuonyesha Wananchi wa Dodoma hawana uelewa wa ugonjwa huo.
Hapo chacha!
Post a Comment