"Yesu harudi duniani mara ya pili "Kadinali Giorgio Salvadore alisema


MSEMAJI kutoka Vatican ameshangaza kutangaza rasmi kuwa kurejea kwa Yesu Kristo mara ya pili kunaweza kukosekana baada ya kusubiriwa sana, japo akiwarai waumini kuendelea kuwa na imani

Kadinali Giorgio Salvadore alisema kuwa maadhimisho ya 1981 katika Jiji la Vatican yatakuwa ya mwisho, kuhusiana na kusubiri Yesu kurejea duniani.

“Tunahisi kuwa Yesu harudi duniani tena kulingana na jinsi mambo yanaonekana,” akasema Giorgio, “Imekuwa miaka mingi. Huenda anafanya mambo mengine ya muhimu kwa watu mahali pengine.”

Alikuwa akisema haya kutokana na hadithi ya Biblia kuwa miaka 2000 iliyopita, Yesu aliahidi wafuasi wake kuwa atarejea tena.

“Kuna maboma mengi huko anakoishi baba yangu, na ninaenda kuyaandaa kwa ujio wenu. Kila kitu kikiwa tayari, nitarejea kuwachukua ili muwe name milele,” Yesu akaahidi wafuasi wake, katika kitabu cha Yohana 14:1-3.

Lakini mkatoliki huyo wa Vatican alidai kuwa wakati alipokuwa akisema maneno hayo “huenda alikuwa akinywa mvinyo.”

“Sote tunaweka ahadi ambazo hatuwezi kutimiza tunapokuwa walevi. Yesu alikuwa hivyo tu,” akasema Salvadore.

Kanisa hilo sasa limesema kuwa litaangazia kujenga heshima yake duniani, japo bila kupoteza matumaini kuwa Yesu anaweza kuja tena.

No comments